



Baadhi ya wanahabari wakichukua taarifa za tamasha la upendo wa mama
Kampuni ya Makundi Production ya jijini Arusha iko katika maandalizi ya kufanya tamasha kubwa la aina yake litakalo julikana kwa jina la UPENDO WA MAMA ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba 2014 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka Kenya, Sara K, na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.
Lengo la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA linalengo la kutoa Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo waliyonao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya watoto.
Studio ya Mkundi nakamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.