PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MKUNDI PRODUCTION YAJIPANAGA KUWAKWAMUA WAKINA MAMA JIJINI ARUSHA .
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Ni katika hali ya kuikumbusha jamii umuhimu wa mazazi katika maisha ya kila siku hasa kwa upande wa mama ambapo Mkundi Pr...

 



SAM_0646
Ni katika hali ya kuikumbusha jamii umuhimu wa mazazi katika maisha ya kila siku hasa kwa upande wa mama ambapo Mkundi Production imeandaa tamasha kubwa la injili ambalo linajulikana kama upendo kwa mama.


Tamasha hilo ambalo litafanyika mwezi wa 11 katika viwanja vya Shekh Abed Jijini Arusha litahuduriwa na waimbaji mbalimbali maarufu wa nyimbo za injili kama vile Upendo Nkone,Christina Shusho,Martha Mwaipaja,Baraka Massa,Eng Carlos, Sarah K kutoka Kenya Pamoja na mama wa Chaguo langu.
 
Lengo hasa la Tamasha hilo ni kuwasaidia Wakina mama ambao wanaishi katika mazingira magumu, Ikiwemo kuwapatia mtaji  ili waweze kujikwamua kiuchumi pamoja na kumudu gharama za maisha.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mkundi Production yenye maskani yake Mkoani Arusha Njiro,Engineer Carlos Dionis Mkundi ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Injili amesema kuwa amepata msukumo wa kuandaa tamasha hilo ili kuwakumbusha watu kuwa Mama ni mtu wa kuthaminiwa katika jamii hivyo anapaswa kusaidiwa.

Licha ya hayo pia amesema kuwa  jamii nyingi zimekuwa haziwajali wakina mama wala kuwapa uzito wa heshima unaostahili hivyo ni wakati sasa wa kila mtu kuhakikisha  wanawasaidia wakina mama,ikiwemo kuwaepusha na majanga ambayo yatapelekea kunyanyasika.

Sambamba na hayo pia katika Tamsha hilo kubwa kabisa kuwai kutokea katika mkoa huo ikiwashirikisha wasanii kutoka Kenya na Tanzania Pia Matumaini na Kiwewe watatumbuiza siku hiyo pamoja na ibaada ya kuwaombea Wakina Mamama.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top