Mbunge
wa Kawe kupitia chama cha Chadema, Halima Mdee, akipandishwa katika
gari la Polisi baada ya kukamatwa akiongoza maandamano ya Wanawake wa
Chadema (BAWACHA) yaliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, kwa kile
kilichodaiwa kuwa maandamano hayo hayakuwa na uhalali, ambapo maandamano
hayo yalikuwa yakienelea Ikulu. Mbunge huyo anataajia kupandishwa
kizimbani kujibu tuhuma zinazo mkabili wakati wowote kuanzia leo.
Halima Mdee akibishana na Askari baada ya kupandishwa kwenye gari la Polisi...
Kinamama wa BAWACHA wakiandamana...na mabango...
Askari akimdhibiti mmoja kati ya waandamanaji......
Chini ya ulinzi....
Baadhi ya kina mama wakizungumza na askari kujaribu kuwaelewesha kuhusu maandamano hayo bila mafanikio..
Halima Mdee akidhibitiwa chini ya ulinzi.......
Mmoja wa waandamanaji akidhibitiwa..
Post a Comment