MKURUGENZI
wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group Ruge Mutahaba,(wanne
kushoto) akiongea na
baadhi ya wakazi wa Dodoma mjini (hawapo pichani) waliohudhuria Semina
ya Kamata
Fursa ndani ya Ukumbi wa Royal Village mapema jana,ambapo aliwaeleza
wakazi hao namna ya kuwapatia mbinu mbalimbali za kujikwamua kupitia
rasilimali zilizopo ndani ya mkoa huo wa Dodoma.
Msemaji
kutoka GS1, Pius Mikongoti akiwalezea wakzi wa Dodoma namna ya
kunufaika kupitia huduma zitolewazo na GS1, hasa katika mfumo wa kutumia
Barcode.
Msanii
wa kughani Mashairi Mrisho Mpoto akiwapa historia yake ya
mafanikio na namna alivyoweza kutumia fursa hadi kufikia hapo alipo kwa
sasa.
Afisa
Utekelezaji na mipango wa NSSF Ally Mkulemba akitoa semina kwa wakazi
wa Dodoma, huku akiwapa mbinu za kutumia fursa katika kusongesha
mafanikio kupitia mikopo mbalimbali itolewayo na Shirika hilo mapema jana
ndani ya Ukumbi wa Royal Village.
Mrisho
Mpoto akimkabidhi kifaa cha kupimia magari mmoja wa wakazi wa Dodoma
Beatrice Chilewa (kulia), muda mfupi baada ya kujishindia moja ya swali
lililoulizwa na msemaji wa GS1, Pius Mikongoti, ambalo lilikuwa
likimtaka ataje nchi tatu za Kusini mwa Jangwa la Sahara zinazotoa
Barcode na namba za utambulisho wa nchi hizo, wa kwanza kutoka kushoto
ni Mkurugenzi wa kampuni ya Josekazi Auto Garage ambaye ndiye mmiliki
wa kifaa hicho cha kupimia magari.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Josekazi Auto Garage, Joseph Mgaya akiwaeleza wakazi wa
Dodoma namna alivyotumia fursa na kumpelekea kumiliki kampuni hiyo
inayojishugulisha na huduma za kutengeneza A/C za magari na Ndege na
namna alivyo wekeza mpaka sasa,ambao amekuwa akitumia vifaa vya kisasa
kikwemo kifaa kinachoweza kupima magari yote
na kujua matizo kwa haraka.
Baadhi
ya wakazi wa Dodoma waliojitokeza kusikiliza mafunzo mbalimbali kwenye
Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal
Village,nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Msanii
wa Bongo Fleva Mwasiti Almasi akiwaeleza wakazi wa Dodoma
namna alivyotumia Fursa iliyopo kwenye muziki na kufanikiwa kuwekeza
baadhi ya mambo kupitia mafao mbalimbali yatolewayo na Shirika la NSSF.
Sehemu
ya watu waliojitokeza kwenye Semina ya Kamata Fursa iliyokuwa
ikifanyika ndani ya Ukumbi wa Royal Village,mjini Dodoma hapo jana.
Mmoja
wa wanasemina hao akiuliza swali lililotokana na mafunzo yaliyokuwa
yakitolewa na wasemaji mbalimbali wa Semina ya Kamata Fursa muda mfupi
kabla ya kumalizika kwa semina hiyo.
Meza
kuu ya watoa mada ya Kamata Fursa wakifuatilia na kusikiliza baadhi ya
maswali yaliyokuwa yakiulizwa na washiriki wa semina hiyo.
Mmoja
wa akina Mama ajishughulishae na shughuli za ujasiliamali katika suala
zina la ubunifu wa mavazi,aliyejitambulisha kwa jina moja la
Neema,akimkabidhi zawadi ya shati msanii wa kughani Mrisho
Mpoto,alilolibuni mwenyewe.
Post a Comment