HABARI ZA HIVI PUNDE:Katibu Mkuu CPA, na aliyewahi kuwa mbunge wa sengerema Dk William Shija amefariki dunia
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola (CPA), Dk William Shija amefariki dunia jijini London, Uingereza.
Dk Thomas Kashililah ambaye ni Katibu wa Bunge, amethibitisha juu ya kifo hicho. Hata hivyo alisema ofisi yake ilikuwa haijapata taarifa kamili juu ya chanzo cha kifo.
Kifo chake kimetokea wakati mkutano Mkuu wa 60 wa CPA ukiwa umeanza, Oktoba 2 na ukitarajiwa kumalizika Oktoba 10 mwaka huu, jijini Younde, Cameroon.
Dk Shija aliyezaliwa mwaka 1947, aliwahi kuwa kwenye Baraza la Mawaziri na Mbunge wa Sengerema kabla ya mwaka 2005. Na pia mhadhiri Chuo cha Nyegezi ambacho sasa hivi ni Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino kabla ya kuingia kwenye siasa.
Aliteuliwa Septemba 9, 2006 kushika nafasi hiyo ya ukatibu mkuu kwenye umoja wa mabunge ya jumuiya.
Anatajwa kuwa mwafrika wa kwanza kuteuliwa kushika nafasi hiyo aliyoitumika tangu Januari Mosi, 2007 akimrithi Denis Marshall wa New Zealand.
Tangu ateuliwa katika wadhifa huo, amekuwa akiishi London.
Mei mwaka huu, Mtendaji huyo wa CPA alikuwa nchini ambako katika semina iliyoandaliwa na umoja huo, alitaka Bunge la nchini, kutengeneza sheria zitakazosaidia wabunge kusimamia matumizi ya serikali na pia kuadhibu watumishi wa umma wanaofuja fedha za umma.
Alimkabidhi Spika Anne Makinda kitabu ‘Followingi the Money’ (kufuatilia fedha) ambacho kwa mujibu wake, kinafundisha namna ambavyo bunge linaweza kufuatilia matumizi ya Serikali Kuu kuona kama yanazingatia pato na sheria. Katika semina iliyoandaliwa CPA, Dk Shija alisema miongoni mwa majukumu ya bunge ni kufuatilia bajeti inayopitishwa kila mwaka
Post a Comment