PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: ARUSHA YAAMKA NA SIMANZI KUBWA BAADA YA AJALI MBAYA YA HIACE ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU 12
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
 Kwa taarifa ya kusikitisha tuliyo ipata muda huu ambayo bado haijathibitishwa inadai kwamba kuna ajali mbaya imetokea katika eneo l...

 Kwa taarifa ya kusikitisha tuliyo ipata muda huu ambayo bado haijathibitishwa inadai kwamba kuna ajali mbaya imetokea katika eneo la Mbele ya Tengeru jirani na Daraja walipo kata migomba ambapo imehusisha gari la daladala ambayo inasemekana kulikuwa na abiria ndani na wengi wamepoteza maisha.


 
 
Ajali hiyo ilihusisha daladala linalofanya safari zake kati ya Arusha mjini na Usa river na lori la mafuta liliokuwa linaelekea Daresalaam  
daladala hiyo yenye namba za usajili T 519 DBJ Iligongana uso kwa uso na lori la mafuta lenye namba za usajili T 905 ACJ lililokuwa linatokea Arusha kwenda Dar es salaam  maeneo ya karibu na tengeru
kwa mujibu wa mashuhuda wanadai kwamba dereva wa hiace alikuwa akiovateki magari ndipo alipokutana na lori likiwa katika mteremko na kushindwa kufunga break na kusababisha kugongangana na hiace na kusababisha vifo vya watu kumi na mbili papo hapo ambapo wa kike ni sita na wa kiume ni sita
inasemekana derva wa hiace aliruka na kufanikiwa kupona na mtoto mmoja wa shule aliyeruka toka katika hiace hiyo
mpaka jana jioni marehemu  waliokuwa wametambulika na ndugu zao ni ZAKIA KITUNGA, LETISIA RUHANGISA, SIMON WILENGA ambaye kondakta  wa hiace hiyo na KUNDAELI KAAYA NA MKEWE ELI KAAYA
marehemu wengine saba walikuwa hawajatambulika mpaka jana usiku miilim yao imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Arusha MOUNT MERU
.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top