MSAFARA WA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR WAPATA AJALI, MAALIM SEIF ANUSURIKA
Gari aliyokuwa amepanda MAALIM SEIF ikiwa imeharibika vibaya
Habari zilizotufikia mda huu Zinasema MSAFARA wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad umepata Ajali mbaya Mkoani Mwanza na kupelekea Viongozi mbalimbali wa Chama hicho kuwa na hali mbaya.
Vilevile Mkurugenzi huyo wa Habari wa Chama hicho alisema kwa sasa Majeruhi hawo wamekimbizwa kwenye Hospitali ya Bugando kupatiwa matibabu na hali yao inaendelea vizuri isipokuwa Katibu chama cha Cuf kutoka Wilaya ya Nyamagana Rehema Mwenda hali yake sio Nzuri kutokana na kupoteza Fahamu
Mkurugenzi wa habari wilaya’na MH SHIDO Ambae ni mwenyekiti wa serikal ya mtaa uliyopo kata ya miringo,wameumia vibaya wamelazwa hospitali ya BUGANDO
Akithitisha kutokea kwa Ajali hiyo wakati anaongea na Mwandishi wa Mtandao huu, mda huu kwa njia ya simu kutoka Mkoani Mwanza kwenye Ajali hiyo, Naibu Mkurugenzi wa Habari kutoka Chama cha Wananchi CUF bwana Kambaya alithibitisha kutokea kwa Ajali hiyo na kusema Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Maalim na Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad ajadhurika na yuko salama bali waliodhurika na Ajali hiyo ni viongozi wa chama hicho,
Rehema Mwendaalikuwa kwenye msafara huo aiugulia maumivu
“Ni kweli Msafara wa Makamu wa rais na Katibu mkuu Taifa umepata ajali ila yeye yuko salama,lakini viongozi wetu wa chama akiwemo katibu wa Chama cha Wananchi CUF Wilaya ya Nyamagana Be Rehema Mwenda Pamoja na Mkuu wa Kitengo cha cha Habari wa chama Chetu wilaya ya nyamagana Hassan Shido ndio wamepata majeraha kutokana na Ajali hiyo,”alisema Kambaya.
Kambaya alizidi kusema Ajali imetokana na Dereva wa Gari aina Scania kwenda kuligonga Gari lilokuwa limewabeka viongozi hao,ambapo gari hilo lilikuwa la nne kutoka gari lililombeba Maalim Seif kwenye msafara huo.
Post a Comment