MBUNGE wa Nzega kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM, Dkt.
Hamisi Kigwangala, ametangaza kugombea urais kwenye uchaguzi ujao wa mwak 2015.
Kigwangala ambaye ni daktari wa binadamu, alitangaza
nia yake hiyo leo mbele ya waandishiw a habari kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro Kempisk jijini
Dar es Salaam, na hivyo kupanua wigo wa wana CCM vijana kutangaza kuwania
wadhifa huo mkubwa kabisa nchini.
Kijana mwingine kutoka chama hicho ambaye tayari
alitangaza kuwania nafasi hiyo ni Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba.
Wengine wanaodaiwa kutaka kuwania nafasi hiyo ingawa
bado hawajatangaza rasmi ni pamoja na Mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowasa,
Frederick Sumaye, na waziri mkuu wa sasa Mizengo Pinda.
Katika orodha ya wanaotamani kuwania nafasi hiyo ni
pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe,
Mwenyekiti wa Bunge Maalum lka Katiba, Samwel Sitta
|
Post a Comment