Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi
mfawidhi, Gilbert Ndeuruo, wakili wa serikali, Ahmed Stambuli, alisema kuwa
Shitambala anashitakiwa kwa kosa la kuingia kwa jinai kinyume cha kifungu
namba 79 ya mwaka 2014 cha kanuni ya adhabu sura ya 16.
Alisema kuwa mshitakiwa kwa nyakati
tofauti kati ya Juni 18, 2012 na Novemba 28, 2013 aliingia na kujenga katika
viwanja namba 27 na 28 ambavyo vinadaiwa kuwa ni mali ya raia wa Tanzania
mwenye asili ya kiasia aliyefahamika kwa jina la Jaswinder Palsingh.
Shitambala ambaye alikuwa akitetewa na
Wakili wa kujitegemea Tasco Luambano alikana shitaka hilo ambapo Hakimu Ndeuruo
alisema kuwa dhamana ya Mshitakiwa iko wazi ikiwa atatimiza masharti ya kuwa na
mdhamini mmoja na ahadi ya fedha kiasi cha sh. milioni 1.
Kwa upande wake wakili wa serikali
Stambuli alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba iko tayari
kuanza kusikilizwa na kuiomba mahakama ipange tarehe ya kuanza kuisikiliza kesi
hiyo.
Hakimu Ndeuruo aliahirisha kesi hiyo
hadi Septemba 10 ambapo itaanza kusikilizwa rasmi.
Alisema kuwa mteja amejenga katika eneo
ambalo wamejenga watu wengine wapatao 400 na kuwa hata hivyo kesi hiyo imemhusu
mteja wake pekee hali ambayo inaonesha nia mbaya iliyofanywa na mlalamikaji
dhidi ya mteja wake.
Post a Comment