Mkurugenzi mtendaji wa TAHA, Jackline Mkindi akiwaeleza wadau
wa Kilimo waliohudhuria kuwa ni muda mrefu kilimo cha mazao ya Maua,
Matunda, mboga mboga, viungo, mbegu na viazi kimesahaulika na kwamba ni
kilimo kinachoweza kumkomboa mkuilima kutokana na urahisi wa ulimaji
wake aliwasisitiza waendeleze Kilimo hicho.
Meza Kuu
Wadau Mbalimbali waliohudhuria katika Mkutano huo
WAZIRI
Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda ameitaka taasisi ya Kilimo cha
mbogamboga(Tanzania Horticultural Association)TAHA kuongeza juhudi za
kutoa elimu kwa wakulima.
Rai
hiyo aliitoa juzi katika kongamano la Uwekezaji lililofanyika katika
ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya ambapo alikuwa mwenyekiti wa kongamano
hilo.
Waziri
Mkuu mbalo na kuwataka TAHA kuongeza juhudi pia alisifu juhudi zao
katika kuinua kilimo na matumizi ya fursa za uwekezaji kwa wakulima.
Akizungumza
katika Kongamano hilo, Mkurugenzi mtendaji wa TAHA, Jackline Mkindi,
aliwaambia wadau wa Kilimo waliohudhuria kuwa ni muda mrefu kilimo cha
mazao ya Maua, Matunda, mboga mboga, viungo, mbegu na viazi
kimesahaulika na kwamba ni kilimo kinachoweza kumkomboa mkuilima
kutokana na urahisi wa ulimaji wake.
Alisema
wakulima inabidi waelimishwe kuhusu kilimo cha mazao hayo kwa sababu
hakihitaji maeneo makubwa na mtaji wa kutosha bali hulimwa katika eneo
dogo lakini yakilenga soko la nje na sio kulima kwa mazoea kwa ajili ya
matumizi ya nyumbani.
Alisema
ili kilimo cha mazao hayo kiwe na manufaa kwa wakulima wa Nyanda za Juu
kusini na kukidhi mahitaji ya soko la nje inabidi serikali iangalie
Changamoto zianazovikabili viwanja vingine vya ndege katika usafirishaji
wa mazao hayo kama Uwanja wa Kilimanjaro( KIA) na Dar Es Salaam( JIA).
Mkurugenzi
huyo alisema maeneo yanayopaswa kuangaliwa mapema kabla ya kuanza kwa
kilimo cha mazao hayo kwa Uwanja wa Kimataifa wa Songwe ni pamoja na
uwepo wa Ndege kubwa ya kusafirisha mizigo inayoweza kupeleka bidhaa
hizo moja kwa moja sokoni pasipo kuathiriwa.
Aliyataja
maeneo mengine kuwa ni kuwepo kwa eneo kubwa na jengo karibu na Uwanja
wa Ndege kwa ajili ya kupozea mazao hayo ili yasiharibike na sehemu
maalumu ya kushushia mazao hayo na kupakilia kwenye ndege pasipo
kuyabughudhi na kuyaharibu kabla ya kufika sokoni.
Alisema
kutokuwepo kwa vitu hivyo kunapunguza ubora wa bidhaa hizo kama maua
ambayo hayatakiwi kunyauka hadi yanafikishwa sokoni ndipo yanakuwa na
soko la uhakika nje ya nchi.
Aliongeza
kuwa soko la nje ya mazao hayo lipo na linauhitaji mkubwa isipokuwa ni
kuzingatia vigezo vya usafirishaji ili kuyafanya yafike sokoni kama
yalivyotolewa shambani.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbasi Kandoro alisema lengo la
mafunzo hayo ni kujadili namna ya kuwawezesha wananchi kujikita katika
uzalishaji wa mazao ya matunda, mboga mboga na maua ili waweze
kuboresha vipato vyao.
Alisema
pia ni utekelezaji wa agizo la Raisi kuhusu manufaa ya uwanja wa Ndege
kwa kilimo hicho kwa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, ambapo aliwataka
viongozi wenzie kutekeleza kwa vitendo agizo hilo na siyo kuiongea tu
mdomoni.
Post a Comment