PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WASANII WA BONGO MOVIE TINO NA DUDE WAKAMATWA NA POLISI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
WASANII nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Hisan Muya ‘Tino’ hivi karibuni walitiwa mbaroni katika mji wa Kilifi ulio mbel...


WASANII nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’ na Hisan Muya ‘Tino’ hivi karibuni walitiwa mbaroni katika mji wa Kilifi ulio mbele ya Mombasa nchini Kenya baada ya kukutwa wakipiga picha za filamu yao bila kuwa na kibali.
Hata hivyo, waigizaji hao baadaye waliachiwa, ingawa hali ilikuwa ngumu kidogo kwa Tino, ambaye polisi wa Kenya walidai hakuwa Mtanzania, bali ni raia wa Somalia.
Dude alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema liliwatokea kutokana na mazoea ya huku nyumbani ambako hufanya shughuli zao za kupiga picha za filamu zao bila kuhitaji kibali.

Msanii nyota wa filamu Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’.
Yaani tumepata aibu ya mwaka, kwani tulienda kushuti bila kuomba kibali kutokana na mazoea ya huku kwetu Bongo, tulipekuliwa sisi na gari letu, baada ya hapo kibali kikaletwa nikaachiwa lakini Tino waliendelea kumshikilia wakisema ni Msomali mpaka mkuu wa shirikisho la filamu Mombasa alipokuja kuokoa jahazi, ukweli Kenya hakufai, alisema Dude. [Via BongoClanTz]

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top