PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BONANZA LA WANAHABARI ARUSHA LAFANA. PINTO AAHIDI KUSAIDIA KUBORESHA LIJALO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Mabingwa katika mpira wa miguu na mpira wa Pete(Netball)Chuo cha Arusha Journalism Training College(AJTC)wakishangilia ushindi wa o ...



Arusha.Timu ya soka na ya mpira wa pete za Chuo Cha Uandishi wa Habari Arusha (AJTC) juzi zilitwaa ubingwa katika bonanza la tisa la waandishi wa habari Kanda ya Kaskazini.
Katika bonanza hilo, lilifanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kuandaliwa na Taswa Arusha na kampuni ya Ms Unique, jumla ya timu 10 zilishiriki kutoka mkoa wa Arusha na Manyara.
Timu ya soka ya AJTC ilitwaa ubingwa baada ya kuifunga kwa mikwaju ya penati 5-4 timu ya Radio Sunrise, wakati wasichana wa timu hiyo, waliwashinda timu ya chuo cha  uandishi wa habari na maendeleo ya jamii (IMS), magoli 18-5.
Mgeni rasmi katika bonanza Mwenyekiti wa Taswa Taifa, Juma Pinto alikabidhi vikombe na fedha taslimu, ambapo bingwa wa very soka alipewa kikombe, ,fedha taslimu 200,000 na seti ya jezi.
Huku mshindi wa pili soka akipata 100, 000 wakati bingwa wa mpira wa pete alizawadiwa kikombe cha fedha taslimu 100, 000 huku mshindi wa pili akikabidhiwa tsh 50, 000.
Katika bonanza hilo, ambalo lilidhaminiwa na kampuni ya bia nchini, (Tbl), kampuni ya Megatrade Investment, Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro, Cocacola, SBC (T) ltd, AICC, Tanzanite Forever, TANAPA na Alphatel timu nyingine zilizoshiriki ni Radio 5.
Nyingine ni timu ya Arusha One, ORS kutoka mkoa wa Manyara, Salam Club, IMS na  Taswa Arusha Arusha ambayo iliambulia ushindi katika kukamata kuku.
Akizungumza katika bonanza hilo, Pinto alipongeza washindi na viongozi wa Taswa Arusha kwa kazi the nzuri waliofanya.
Pinto pia aliahidi katika maadhimidho ya miaka 10 ya bonanza hilo, mkutano mkuu wa T aswa Taifa utafanyik a Arusha sambamba na tuzo za waandishi bora.
Awali Meneja matukio wa TBl, Chris Sarakana aliahidi Tbl kuendelea kudhamini bonanza hilo kutokana na kuvutia wanahabari na wakazi wengi wa Arusha.
Meneja masoko wa Mega trade, Godluck Kway aliwapongeza wanahabari kwa kushiriki kwa wingi katika bonanza hilo na kuahidi kue kudhamini.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top