TWIGA WA HIFADHI YA RUAHA WAKUMBWA NA UGONJWA USIOJULIKANA A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: TWIGA WA HIFADHI YA RUAHA WAKUMBWA NA UGONJWA USIOJULIKANA Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: Asilimia tisini ya Twiga wote waliopo katika mbuga ya wanyama ya Ruaha wameathiriwa na ugonjwa unaosambaa kwa kasi ambao haujulikani, ki... Asilimia tisini ya Twiga wote waliopo katika mbuga ya wanyama ya Ruaha wameathiriwa na ugonjwa unaosambaa kwa kasi ambao haujulikani, kimeripoti Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine. Taarifa zinasema kuwa wanasayansi wa chuo hiko wakishirikiana na Mamlaka ya Mbuga ya Wanyama Tanzania (TANAPA) wanapambana kuzuia ugonjwa huo ambao tayari umeshaonekana kwenye mbuga nyingine ya Tarangire. Profesa Gerald Msinzo, alisema ugonjwa husababishwa na bakteria na uligunduliwa na maafisa wa TANAPA, ambapo wameonya kuwa hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa kwani wanyama hao ambao ni kielelezo cha taifa na kwa sasa wapo katika hatari kubwa. Alisema kuwa ugonjwa huo una dalili za kuwadhoofisha wanyama, kutokwa kwa vipele kwenye ngozi zao ambavyo hugeuka kuwa vidonda na majeraha kwenye miguu yao. “Ugonjwa huwadhoofisha Twiga na kudhuru uwezo wao kutoka sehemu moja kwenda nyingine na hivyo kuathiri ulaji wao na hata tabia za kushirikiana na wanyama wengine” alisema Profesa Msinzo. Pia aliongeza kwamba vinasaba wa bakteria wanaosababisha ugonjwa huo vimeshapelekwa kwenye maabara za chuo kikuu kwa ajili ya uchunguzi ili kutambua ugonjwa na kupata tiba yake. Hata hivyo, hakuna taarifa kuwa ugonjwa huo unaweza kusambaa na kuweza kuambukiza viumbe wengine kama wanyama, mimea na hata binadamu
Post a Comment