SIKU YA MTOTO AFRIKA ILIVYOFANA JIJINI ARUSHA A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: SIKU YA MTOTO AFRIKA ILIVYOFANA JIJINI ARUSHA Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: Watoto wa shule ya msingi Kilimani iliyoko jijini Arusha wakiwa kwenye gharide maalumu la kuadhimisha siku yao leo katika viwanja vya ... Watoto wa shule ya msingi Kilimani iliyoko jijini Arusha wakiwa kwenye gharide maalumu la kuadhimisha siku yao leo katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume,kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Elimu bora na isiyo na vikwazo ni haki ya mtoto.Watoto nchini wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kufanyiwa vitendo vya ukatili,watoto wa mitaani wanaokosa matunzo na elimu,uhaba wa vifaa katika shule.Picha na Ferdinand Shayo Watoto wa shule ya msingi Kilimani iliyoko jijini Arusha wakiwa kwenye gharide maalumu la kuadhimisha siku yao leo katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume,kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Elimu bora na isiyo na vikwazo ni haki ya mtoto.Watoto nchini wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kufanyiwa vitendo vya ukatili,watoto wa mitaani wanaokosa matunzo na elimu,uhaba wa vifaa katika shule.Picha na Ferdinand Shayo Watoto Kutoka shule mbali mbali za msingi Kilimani zilizoko jijini Arusha wakiwa kwenye gharide maalumu la kuadhimisha siku yao leo katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Karume,kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Elimu bora na isiyo na vikwazo ni haki ya mtoto.Watoto nchini wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo kufanyiwa vitendo vya ukatili,watoto wa mitaani wanaokosa matunzo na elimu,uhaba wa vifaa katika shule.Picha na Ferdinand Shayo Wadau Walaani Ukatili dhidi ya Watoto Na Ferdinand Shayo,Arusha. Wadau mbali mbali wa masuala ya watoto wamelaani vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watoto ikiwemo ubakaji,ulawiti, kupigwa na kutumikishwa kwenye ajira huku wakizitaka mamlaka husika na jamii iwachukulie hatua stahiki wale wanaobainika kufanya vitendo hivyo. Aidha wameeleza kuwa ukatili unaofanya majumbani umekuwa ukinyamaziwa kimya na kumalizika kwa ngazi ya familia bila kufika katika vyombo vya sheria jambo ambalo linasababisha kushamiri kwa vitendo hivyo na kukosa ukomo. Faith Wiliam Swai ni Mkurugenzi wa Asasi inayojihusisha na kupiinga ukatili kwa watoto na kinamama ya (WOCHIVI) amesema kuwa tayari wamemfikisha mahakamani mtu mmoja anayedaiwa kuwabaka watoto wa tatu wa familia moja baada ya kugundua wazazi wao huenda mbali na nyumbani kwa shughuli za utafutaji. Akizungumza katika maadhimimisho ya siku ya mtoto Afrika yaliyofanyika jijini hapa ,Faith amesema kuwa wamekuwa wakishirikiana na wananchi pamoja na serikali katika kubaini matukio hayo na kuwachukulia hatua wahusika ili vitendo hivyo vikome katika jamii. Afisa Ustawi wa jamii wa jiji la Arusha amesema kuwa ili kukomesha vitendo hivyo wamekuwa wakishirikiana na Dawati la jinsia lililopo chini ya jeshi la polisi jambo ambalo tayari juhudi zimeshaanza kuzaa matunda. Maurine Marungi ni Mwalimu katika shule ya msingi Kilimani iliyopo jijini hapa anaeleza kuwa tatizo la watoto wa mitaani limekuwa kwa kiasi kikubwa hivyo ameiomba serikali ,jamii na taasisi binafsi kusaidia kupunguza tatizo hilo. Idda Clay ni mwanafuzi wa shule ya msingi Olasiti anaeleza changamoto zinazowakabili ni pamoja na ukosefu wa lishe bora,vifaa,maktaba,maabara,madarasa ya kutosha,kutolipiwa ada kwa wakati,walimu wenye sifa na kuiomba serikali isaidie kuta Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Arusha Kiomoni Kibamba amesema kuwa wazazi wanapaswa kuwajibika na kuanzia ngazi ya familia na kuwa serikali haitawavumilia wazazi wasiowapatia mahitaji watoto wao na kulipa ada kwa wakati kwa makusudi bila kuwa na sababu za msingi.
Post a Comment