- Walalamikia wingi wa kodi wanazokatwa na riba kubwa za mabenki
- Walalamikia utapeli unaofanywa na vyama vya ushirikia, wizi na ulanguzi wa pembejeo
- Walalamika kupangiwa bei kwa dola,kutolipwa kwa wakati
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya
Sikonge kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM
Sikonge ambapo aliwapongeza kwa juhudi zao za kuleta maendeleo yao
katika ngazi ya wilaya lakini pia alisema wakulima wanatakiwa kusaidiwa
mara moja kuondoa kero zao.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua Album ya kikundi cha
Kwaya cha Umoja Sanaa Group chenye wasanii 27 ambao wanaimba nyimbo za
kuhamasisha Chama cha Mapinduzi wilayani Sikonge mkoa wa Tabora.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa Sikonge
ambapo aliwaambia wawe makini sana na sera za vyama vya upinzani kwani
vyama vingine sera zao si nzuri kwa maendeleo ya Taifa
Mwenyekiti
wa UWT mkoa wa Tabora Mwanne Nchemba akiwasalimu wakazi wa Sikonge
kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndgu Abdulrahman Kinana
uliofanyika Sikonge mkoani Tabora.
Wasanii
wa Kikundi cha Umoja Sanaa Group wakitumbuiza kabla ya kuanza kwa
mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
alihutubia wakazi wa Sikonge mkoani Tabora .Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma orodha ya nyimbo zilizopo kwenye album ya kikundi cha Umoja Sanaa Group cha CCM Sikonge,kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Ndugu Fatma Mwassa akiangalia kasha la album hiyo na katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
Post a Comment