TAMASHA LA MTU KWAO ARUSHA KUSHIRIKISHA MACHIFU 120,MRISHO MPOTO NA WEMA SEPETU KUNOGESHA A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: TAMASHA LA MTU KWAO ARUSHA KUSHIRIKISHA MACHIFU 120,MRISHO MPOTO NA WEMA SEPETU KUNOGESHA Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: chifu Gilbert Isambe akiwa na vazi la kichifu chifu Gilbert Isambe akiwa anaongea na vyombo vya habari pembeni ni mratibu... chifu Gilbert Isambe akiwa na vazi la kichifu chifu Gilbert Isambe akiwa anaongea na vyombo vya habari pembeni ni mratibu wa tamasha la Mtu kwao bi Janeth Jonas Zaidi ya machifu 100 kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini wanatarajia kuuthuria katika tamasha la mtu kwao linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi May 15 hadi 20 mwaka huu katika kiwanja cha kumbu ya sheikh Amri Abeid jijini hapa. Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa Mratibu wa tamasha hilo ambaye ni mkurenzi wa kampuni ya Utamaduni Traning L.T.D Janeth Jonas alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha machifu 120 kutoka katika mikoa mbalimbali na makabila mbalimbali ya hapa nchini. Alibainisha kuwa nia na dhumuni la kuandaa tamasha hili la mtamaduni wetu ni kuweza kuuenzi utamaduni wa mtanzani ambapo ni kuanzia mavazi ya makabila mbalimbali,vyakula pamoja na ngoma kutoka katika makabila yote hapa nchini. “pia katika tamasha hili tumeamua kuwaita machifu mbalimbali l kutoka katika makabila mbalimbali hapa nchini na baadhi ya mchifu ambao watauthuria ni pamoja na chifu kutoka oldmoshi ambaye yeye ameshawasili hapa Arusha kwaajili ya tamasha hili Gerald Mandera ,chifu Gilbert Rugal Isambe kutok a kasulu na wengine wengi wote watakuwepo”alisema Janeth Aidha alisema kuwa katika tamasha hili kila mtu atapata fursa ya kuona ngoma kutoka katika makabila mbalimbali pamoja na kuonja chakula cha kila aina cha makabila ya hapa nchini pamoja na nje ya nchi Alisema kuwa pia katika tamasha hili zaidi ya vikundi vya ngoma 100 vitatumbuiza pamoja na wasanii mbalimbali akiwepo msanii wa ngoma za utamaduni Mrisho mpoto,wema sepetu ,kundi la weusi kutoka Arusha,Jambo Squards ,Dogo janja pamoja na msanii kutoka nchini Kenya Daniel ole Sekuo. Naye mmoja wa machifu ambaye atauthuria tamasha hilo Chiefu Gerald Mandera kutoka oldmoshi alisema kuwa waandaaji wamefanya jambo jema sana kuanda tamasha hili kwani wao ndo wametambua uwepo wa machifu na wameona umuhimu wao mpaka wameamua kuwakusanya pamoja katika tamasha kama hili. Alisema kuwa sasa ivi serekali nayo inawajibu wa kujipanga vilivyo na kutenga siku maalumu kwa ajili ya kufanya tamasha hili kama jinsi wenzetu kutoka katika nchi zingine wanavyo azimisha siku hii katika tarehe hizi na mwezi huu kila mwaka. Aidha alibainisha kuwa kuwakusanya watu mbalimbali kutoka katika tamaduni mbalimbali pamoja na makabila mbalimbali itasaidia kwani inaweza kuwezesha hata nchi kupata vazi la taifa kwani makabila haya yate yanakuja yakiwa yamevaa vazi la ukabila wao na hii itakuwa fursa pekee ya kuweza kuchagua vazi hasili la mtanzanzia. “ni aibu kubwa sana unakuta sisi kama watanzania hadi leo hii atuna vazi linaloweza kutuwakilisha sisi kama watanzania na ukiangalia wenzetu wa n je ya nchi wanamav azi yao ya kiutamaduni ambao ukimuona tu mtu amevaa unajua katoka katika kabila Fulani ,naitanishangaza sana kuona mtu anauzarau utamaduni wake na anauweka mbele utamaduni wa kigeni “alisema chifu Gilbert Isambe Aidha alibainisha kuwa hii ni fursa ya watukuja kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo ,akiwasihi wanafunzi wa shulembalimbali pamoja na wanavyuo mbalimb ali kuja katika tamasha hili kushuhudiana kuwaona machifu ambao mud a mrefu walikuwa wanawasoma tu kwenye vitabu bilakuwaona moja kwa moja.
Post a Comment