PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SERIKALI YAPIGA MARUFUKU UINGIZAJI WA KUKU WA NYAMA NCHINI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
“Serikali haijawahi kutoa vibali vya uingizaji wa kuku wala nyama kutoka nje, ili kunusuru wazalishaji wa ndani, na kulinda ajira za wan...


“Serikali haijawahi kutoa vibali vya uingizaji wa kuku wala nyama kutoka nje, ili kunusuru wazalishaji wa ndani, na kulinda ajira za wananchi,”

Serikali imesisitiza uamuzi wake wa kupiga marufuku uingizwaji nchini wa kuku, nyama ya kuku na vifaranga ili kudhibiti ugonjwa ya mafua ya ndege na kulinda wawekezaji wa ndani.
Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani alitoa agizo hilo baada ya kutembelea kampuni ya Tanzania Poulty Farms Limited, inayomiliki shamba la kuku wa nyama na vifaranga lililopo kijiji cha Ngogongare na kiwanda cha uchinjaji kuku kilichopo Mbuguni wilayani Arumeru.
Waziri Kamani alisema Serikali ilipiga marufuku uingizwaji wa kuku wa nyama na vifaranga kutoka nje kutokana na magonjwa ya mafua ya kuku na haijaruhusu uingizwaji huo kwa lengo la kunusuru soko la wazalishaji wa ndani .
“Serikali haijawahi kutoa vibali vya uingizaji wa kuku wala nyama kutoka nje, ili kunusuru wazalishaji wa ndani, na kulinda ajira za wananchi,” alisema
Aaliwapongeza wamiliki wa shamba hilo kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika kuwahudumia kuku, utengenezaji wa chakula cha kuku, kufuga hadi kuchinja na kuhifadhi kwenye majokofu kwa ajili ya kusafirisha kwenda sokoni.
‘’Hii ni teknolojia ya kwanza na ya kisasa kutumika hapa nchini ya kuwahudumia kuku, kuzalisha chakula, kufuga na kuwachinja na kisha kusambaza kwenye soko,’’ alisema
Awali mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tanzania Poultry Farms Limited, Amin Bathawab alisema walianza uwekezaji mwaka 1996 baada ya kuinunua iliyokuwa kampuni ya taifa ya kuku, Napco, ikiwa na kuku 2,000.
Alisema hadi sasa wana kuku wazazi 80,000 na vifaranga 90,000. Hivi sasa wanauza vifaranga nchi nzima kupitia kwa mawakala.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top