MAONYESHO
ya biashara ya bidhaa za Uturuki na Tanzania yaliyofanyika jijini Dar
es Salaam kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, yamevuta watazamaji wengi
kuwa na shauku ya kutembelea mabanda mbali mbali likiwemo banda la
Kampuni ya Jamii Media iliyoshiriki maonyesho hayo, ambao ni wamiliki wa
mitandao maarufu ya mijadala kwa jamii kupitia mitandao ya kijamii,
JamiiForums na FikraPevu nchini Tanzania.
Maonyesho
hayo ambayo yalifanyika kwa siku tatu katika ukumbi huo na kumalizika
leo, mbali na wananchi kujionea bidhaa mbalimbali
kutoka kwa wafanyabiashara kutoka ndani na nje ya nchi baadhi yao
wamejisajili na kuwa wanachama hai katika mtandao wa Jamii Forums ili
kupata faida katika nyanja tofauti/mchanganyiko.
Aidha,
baadhi ya wananchi walio wengi waliotembelea maonyesho hayo walipa
fursa ya kujua namna Jamii Media inavyofanya kazi pamoja na manufaa
yaliyopo kwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwemo JamiiForums na
FikraPevu.
Maonyesho
hayo yalifunguliwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
(TPSF), Dk. Reginald Mengi,Mei 15, 2014 ambapo aliwataka watanzania
kupitia maonyesho hayo kujijifunza kutengeneza bidhaa zenye ubora wa
hali ya juu na zenye bei nafuu kama zilivyo bidhaa zinazotoka nchini
Uturuki.
Dk.
Mengi, aliwataka wawekezaji wa nje ya nchi kuja kuwekeza Tanzania ili
Watanzania wajifunze teknolojia ya viwanda na kuongeza nafasi za ajira
kukuza uchumi, pamoja na makampuni ya Kitanzania kushiriki maonyesho
mbalimbali kama hayo kwani yatawasaidia kutafuta soko la bidhaa zao
kwenda nje ya nchi na pia yatawapa nafasi ya kushiriki katika maonyesho
kwenye nchi nyingine.
Mtandao
wa JamiiForums unatajwa kuwa miongoni mwa mitandao ya kijamii
inayosimamia uhuru wa habari, kuhabarisha na kushirikisha wananchi kwa
habari na matukio katika kila nyanja. Husomwa na watu zaidi ya laki tatu
hadi nne kwa siku na hivyo kuchangia kusambaza habari kwa haraka na
upana kuliko chombo chochote cha mitandao ya Kijamii nchini.
Post a Comment