MAMBO yanazidi kuwa mambo kuhusu ile ndoa ya Mbunge Vicky Kamata
iliyoyeyuka katika dakika za majeruhi, safari hii Risasi Mchanganyiko
limefanikiwa kuwanasa baadhi ya wapambe ambao walitakiwa kuwa kwenye
msafara wa harusi hiyo kutoka kanisani hadi ukumbini.
Wapambe hao walitia timu kwenye wodi aliyokuwa amelazwa Vicky katika
Hospitali ya General iliyopo Tabata jijini Dar es Salaam, Jumamosi
iliyopita (ambayo ndiyo ilikuwa ndoa ifungwe).
WAPAMBE WATATU
Katika idadi ya watu sita waliofika kumjulia hali Vicky, watatu wakiwemo
wanaume wawili ndiyo waliokuwa wamevaa sare ya harusi hiyo ambayo
ingetawaliwa na rangi ya purple ‘papo’ (angalia picha ukurasa wa mbele).
SARE KAMILI
Iilithibitika kwamba sare za shughuli hiyo zilishashonwa, wanaume
waliokuwa mstari wa kusindikiza maharusi walitakiwa kuvaa suti nyeusi
(single button), shati jeupe na tai fupi (necktie) yenye rangi ya papo
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wanawake ambao pia walikuwa kwenye msafara
wa maharusi (ma-maids) walitakiwa kuvaa magauni ya rangi hiyohiyo ya
papo.
KWA NINI WALIVAA HUKU WAKIJUA HARUSI HAIPO?
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wapambe hao walikuwa ndani ya mavazi hayo
kwa sababu walijua baada ya ndoa kuyeyuka, wasingeweza kuvaa siku
nyingine.
“Unajua wale si kwamba walikwenda pale na sare wakijua ndoa ipo, walijua
kabisa kwamba haipo ila sasa kwa sababu ndiyo ilikuwa siku yenyewe
ilibidi wajipigilie tu kama kusafisha hali ya hewa au wengine husema
‘kuoshea’ jina,” kilisema chanzo.
UKUMBI WADODA
Waandishi wetu Jumapili iliyopita walikwenda mbele zaidi kwa kufika
kwenye Hoteli ya Hyatt Regency The Kilimanjaro ya jijini Dar es Salaam
ambako shughuli ya ndoa hiyo ingefanyikia.
Mfanyakazi mmoja ambaye aligoma kutaja jina kwa sababu si msemaji wa
hoteli hiyo alisema ukumbi ambao ulikuwa utumike kwa harusi ya Vicky
Kamata uitwao Kili Marquee ulilala doro baada ya wahusika kuweka wazi
kwamba hakuna harusi tena.
“Ukumbi ulilala mtupu, taarifa zilishakuja mapema kwamba hakuna harusi,” alisema mfanyakazi huyo.
Alipoulizwa ni kwa nini wasikodishe kwa mtu mwingine, mfanyakazi huyo alisema si utaratibu wa hoteli hiyo.
“Wale walishalipia, sasa ukisema ukodishe kwa wengine kwa sababu harusi
haipo, je, ingetokea harusi ikaja ghafla na kukuta wateja wengine? Si
ingekula kwetu?” Alisema mfanyakazi huyo.
MILIONI 40 ZA MCHANGO ZATATIZA
Kuna habari kwamba, zaidi ya shilingi milioni arobaini ambazo zilikuwa za mchango wa harusi hiyo zimetoweka kusikojulikana.
Fedha hizo zilichangwa na wadau mbalimbali katika kufikia kile kiasi cha
shilingi milioni 96 ambazo zilidaiwa tangu awali kwamba ndizo
zingefanikisha shughuli nzima ya harusi hiyo iliyotarajiwa kuwa ya
kifahari.
BWANA HARUSI HAJULIKANI ALIPO
Ili kupata uwiano sawa wa habari hii, juzi Jumatatu waandishi wetu
walimtafuta mwanaume aliyetarajiwa kufunga ndoa na Vicky, Charles kwenye
ofisi ya kampuni moja ya simu za mkononi, Kijitonyama jijini Dar lakini
baadhi ya wafanyakazi walisema ana wiki mbili hajakanyaga kazini.
“Huyu bosi hajakanyaga hapa wiki mbili, hayupo,” alijibu mfanyakazi mmoja.
Risasi Mchanganyiko: “Hajakanyaga kivipi? Kasafiri, yuko likizo au?”
Mfanyakazi: “Aliandika barua ya kuomba mapumziko ya wiki mbili kwa hiyo hatujui yuko wapi kwa sasa.
NYUMBANI KWA VICKY
Baada ya kutoka ofisini kwa bwana harusi, wanahabari wetu walitinga
nyumbani kwa bibi harusi Vicky Kamata, Sinza ya Vatican, Dar na
kukumbana na mlinzi getini ambaye alisema mgonjwa huyo aliruhusiwa
kutoka hospitali saa mbili usiku wa Jumapili lakini alikuwa amelala na
haruhusiwi kuzungumza na mtu yeyote zaidi ya kupumzika.
“Mheshimiwa karudi jana usiku saa mbili lakini haruhusiwi kuzungumza na watu, amelala,” alisema mlinzi huyo.
About Author

Advertisement

Related Posts
- Magazeti ya Tanzania October 1, 2016 kuanzia, Udaku, Hardnews na michezo01 Oct 20160
October 1 2016 naanza kwa kukusogezea po...Read more »
- AJTC yang'ara kwa kutoa watangazaji na waandishi bora Africa mashariki10 Mar 20160
Hii ni habari njema kwa wale waliomaliza kidato cha nne na sita.Unaweza kujiunga na chuo cha Uandish...Read more »
- Millard Ayo 'Mimi ni Miongoni Mwa Wanafunzi Waliofeli Kidato cha Nne Lakini Niliinuka na Kuendelea'09 Mar 20160
Mtangazaji mahiri wa kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM Millard Ayo baada ya ku...Read more »
- TAASISI YA TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) YAZINDUA KAMPENI YA UWIANO WA KIJINSIA..18 Feb 20160
Rais wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) (TWA), Irene Kiwia (katikati...Read more »
- Mhe. Luhaga Mpina Atembelea Kituo cha Afya Fuoni Kibondeni na Skuli ya Msingi Kitongani Fuoni Kuangalia Ahadi ya Ujenzi wa Madarasa ya Skuli hiyo Yaliotolewa Ahani na Rais Mstaaf Jakaya Kikwete.12 Feb 20160
Kituo cha Afya kilioko Fuoni Kibondeni ambacho kilitembelewa na Mhe Luhaga Mpina katika Jimbo la ...Read more »
- UN YAIPONGEZA TANZANIA KWA JUHUDI ZINAZOFANYWA NA SERIKALI KUKABILI UKATILI DHIDI YA WANAWAKE11 Feb 20160
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.