Kikosi
Kazi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, kimebaini njia mpya ya
wasafirishaji, ambapo sasa wanapitisha nchi jirani ili wasigundulike
kirahisi na baadaye huzifuata.
Njia wanazotumia wasafirishaji hao ni kupitisha mizigo yao kwenye miji ya Maputo, Kampala na Nairobi.Mkuu
wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Kamanda Godfrey Nzowa alisema
wasafirishaji hao huagiza dawa hizo kutoka sehemu mbalimbali na
kuzipeleka kwenye nchi ambazo hazina sheria kali.
alisema.
Alisema kwa hali hiyo, sasa wasafirishaji wa dawa hizo wanaharibu njia za kawaida za ndege.
alisema.
Alisema
kuanzia Januari hadi Mei mwaka huu, wamekamata kilo 250 za dawa za
kulevya aina ya heroine na kilo tisa za cocaine na watuhumiwa 22
kufikishwa mahakamani.
Alisema watuhumiwa 16 kati ya hao ni raia wa kigeni na wanne kutoka nchini, ambao walikamatwa na dawa zenye thamani kubwa.
Watuhumiwa
waliokamatwa na dawa zenye thamani zaidi ya Sh10 milioni, kesi zao
zitasikilizwa Mahakama Kuu. Raia wa kigeni waliokamatwa na dawa za
kulevya, Liberia (4), Palestina (4), Kenya (1), Nigeria (1), Marekani
(1) na Iran (8)
Post a Comment