Wahamiaji haramu 47 wakamatwa mkoani Kilimanjaro! A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: Wahamiaji haramu 47 wakamatwa mkoani Kilimanjaro! Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: IDARA ya Uhamiaji Mkoani Kilimanjaro, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani humo, inawashikilia wahamiaji haramu 47 raia wa nchi ya ... IDARA ya Uhamiaji Mkoani Kilimanjaro, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani humo, inawashikilia wahamiaji haramu 47 raia wa nchi ya Ethiopia, kwa tuhuma za kuingia nchini kinyume cha Sheria.Mbali na wahamiaji haramu hao pia Idara hiyo inamshikilia mtu mmoja raia wa hapa nchini Benjamini Saimon (28) mkazi wa Kibamba mkoani Dar es salam, kwa tuhuma za kuhusika na kuwasafirisha wahamiaji haramu hao.Kwa mujibu wa Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Kilimanjaro, Johannes Msumule, alisema wahamiaji hao walikamatwa April 3, mwaka huu, majira ya saa 9:30 usiku katika eneo la Chekereni katika kata ya Kahe Wilaya ya Moshi barabara kuu ya Moshi/Tanga.Amesema raia hao ni wa Ethiopia, ambapo walikamatwa wakiwa kwenye gari lenye namba T216 ASU aina ya Fuso, wakiwa kwenye harakati za kutaka kusafiri kwendaAfrika kusini, kulingana na kwamba walikamtwa na Askari pamoja na Maafisa wa Iadara ya uhamiaji waliokuwa doria katika eneo hilo, na taarifa ilizotolewa na raia wema. “Mwezi wa tano tunaenda katika maeneo ya mipakani kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi kule, kama Kilobo, Kileo, Holili, Kifaru na maeneo yote ili tuweze kufanya hii kazi kwa kushirikiana na wao” alisema MsumuleHata hivyo alisema kwa sasa Idara hiyo imejipanga vizuri ili kuweza kutokomeza tatizo la wahamiaji haramu, ambapo kwa sasa wameanza kufuatilia ili kuwabaini watu ambao wamekuwa wakijihusisha na kazi ya kuwasafirisha wahamiaji haramu.Alisema katika kipindi cha miezi mitatu ya mwaka huu, jumla ya wahamiaji haramu 216 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali nchini. huku jumla ya Kesi 12 zikiwa zimefikishwa Mahakamani ambapo kesi moja imemalizika na nyingine 11 bado zinaendelea kushughulikiwa.\
Post a Comment