PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TFDA yateketeza Shehena ya Mikate ya Kiwanda cha 'Manyara Loaf'!!!!
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kaskazini, imetekeza shehena ya Mikate katika Kiwanda cha Mikate cha Manyara Loaf cha mkoa...


MAMLAKA ya Chakula na Dawa (TFDA) Kanda ya Kaskazini, imetekeza shehena ya Mikate katika Kiwanda cha Mikate cha Manyara Loaf cha mkoani Arusha, baada ya kugundua ya kuwa Mikate hiyo inatengezwa chini ya kiwango na katika mazingira yasiyo salama hali inayohatarisha afya ya watumiaji.

Aidha,  TFDA inamtafuta mmiliki wa kiwanda hicho ambaye alitoweka baada ya kuarifiwa kuhusu wakaguzi kufika kiwandani kwake.
Kaimu Meneja wa TFDA Kanda ya Kaskazini Salma Mhando, amesema Kiwanda hicho kilifungwa na Mamlaka hiyo lakini wahusika wakaendelea kuzalisha mikate bila kujali kwamba kiwanda hicho hakijakidhi masharti waliyopewa na mamlaka hiyo. Kiwanda hicho kimefungwa na mmiliki atachukuliwa hatua za kisheria atakapopatikana, kwa mujibu wa TFDA.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyakazi waliokutwa katika kiwanda hicho,walisema hatua ya kukifunga Kiwanda hicho itawaathiri kimaisha kwani hawana njia mbadala ya kujikimu ikizingatiwa kwamba hawajalipwa mishahara yao kwa muda mrefu. TFDA iliwaambia wafanyakazi hao haina mamlaka ya kuingilia kuhusu malipo yao.
Baadhi ya Wananchi Mkoani humo wameitaka Serikali kuboresha Sheria ya Chakula kuongezewa Makali, ili kuweza kuwabana wale wote wanaoenda kinyume na Sheria hiyo ili kunusuru Afya zao pindi watumiapo bidhaa zisizokidhi Vigezo.

Sheria ya Chakula inasema nini kuhusu suala hili
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ilianzishwa chini ya kifungu 4(1) cha sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Na. 1 ya mwaka 2003 na iliundwa baada ya Bunge kufuta sheria ya Dawa na Sumu na sheria ya Kudhibiti Ubora wa Vyakula zote za mwaka 1978.
Moja ya majukumu ya TFDA ni pamoja na kukagua viwanda vya utengenezaji na maeneo ya kuuzia bidhaa zinazodhibitiwa na mamlaka ili kuhahikisha viwango vilivyowekwa vinafikiwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top