PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Kodivaa yaafiki kushitakiwa mpambe wa Gbagbo ICC
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Charles Blé Goudé, mmoja wa viongozi waandamizi wa utawala wa Laurent Gbagbo  Serikali ya Kodivaa imetangaza kuunga mkono kushita...

 
  Charles Blé Goudé, mmoja wa viongozi waandamizi wa utawala wa Laurent Gbagbo 

Serikali ya Kodivaa imetangaza kuunga mkono kushitakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, mpambe wa rais wa zamani za nchi hiyo Laurent Gbagbo. Hayo yalithibitishwa jana na Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Mamadou Gnénéma Coulibaly, baada ya kumalizika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichohudhuriwa na Rais Alassane Ouattara na kuongeza kuwa, serikali ya Yamoussoukro imeafiki kumkabidhi Charles Blé Goudé mmoja wa viongozi waandamizi wa utawala wa Laurent Gbagbo kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC. Mamadou Gnénéma ameongeza kuwa, tayari serikali imekwishachukua hatua za lazima za kufanikisha zoezi hilo. Waziri huyo wa sheria nchini Ivory Coast amemtuhumu Charles Blé Goudé kuwa alitumia jumuiya ya wanafunzi nchini humo (FESCI), kuzusha machafuko makubwa katika vyuo vikuu vya nchi hiyo wakati wa utawala wa Gbagbo ambaye hadi sasa bado anashikiliwa na mahakama hiyo ya ICC. Kushambuliwa magari ya Umoja wa Mataifa mwaka 2010 nchini humo, ni miongoni mwa tuhuma zinazomkabili jenerali huyo wa zamani wa utawala ulioipita. Kodivaa iliingia katika vita vya ndani baada ya Laurent Gbagbo kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Rais wa sasa Alassane Ouattara. Machafuko ambayo yalipelekea kuuawa zaidi ya watu 3000 na wengine wengi kujeruhiwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top