Safari za ndege mjini Tripoli, Libya, zasimamishwa A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: Safari za ndege mjini Tripoli, Libya, zasimamishwa Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: Safari za ndege nchini Libya zimesimama b... Safari za ndege nchini Libya zimesimama baada ya kutokea shambulio la maguruneti kwenye uwanja wa ndege wa mjini Tripoli mapema leo asubuhi na kusababisha hasara kubwa uwanjani hapo. Duru moja ya habari ambayo haikutaka kutaja jina lake imesema kuwa, hadi sasa safari za ndege katika uwanja wa ndege wa Tripoli, zimesimama hadi kutakapotolewa taarifa kamili, baada ya uwanja huo kushambuliwa kwa maguruneti mawili katika barabara za kupaa na kutua ndege. Chanzo hicho kimeongeza kuwa, taarifa za awali zinasema kwamba, safari za ndege katika uwanja huo, zitaanza tena siku ya Jumatatu. Ni vyema kuashiria hapa kwamba, tangu ulipopinduliwa utawala wa Kanali Muammar Gaddafi, uwanja wa ndege wa Tripoli ulikuwa ukidhibitiwa na wanamgambo wa zamani wa Zintan, mji ulio umbali wa kilometa 170 kusini magharibi mwa mji mkuu, Tripoli. Hii ni katika hali ambayo, viongozi wa Libya hawajaweza kuyanyang'anya silaha makundi ya wanammgambo wa zamani, huku makundi hayo yakiwa bado yanadhibiti maeneo muhimu sana ya serikali nchini Libya.
Post a Comment