Wanafuzi 17 wafungwa miaka 14 jela nchini Misri
Mahakama moja nchini Misri, imewahukumu kifungo cha miaka 14 jela wanafunzi 17 wa nchi hiyo kwa tuhuma za kuzusha vurugu, kuwashambulia askari na kukishambulia Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar.
Tuhuma nyingine zilizokuwa zinawakabili wanafunzi hao ni pamoja na kuharibu mali za umma. Hata hivyo na licha ya mahakama hiyo kutoa hukumu hiyo, lakini wanafunzi hao hadi dakika ya mwisho wameendelea kupinga tuhuma hizo. Mbali na kifungo, wanafunzi hao wametakiwa kulipa faini ya dola elfu 13 za Kimarekani. Wakati huo huo, duru za habari nchini Misri zimetangaza habari ya maafisa usalama wa nchi hiyo kumzuia kushuka ndege katika uwanja wa kimataifa wa mjini Cairo mapema leo, mwanaharakati mmoja wa haki za binaadamu raia wa Ufaransa. Kwa mujibu wa vyombo vya usalam nchini humo, jina la mwanaharakati huyo aliyekuwa ametokea nchini Uturuki kwenda Misri, liko katika orodha ya majina ya watu waliopigwa marufuku kuingia nchini humo. Baada ya kuzuiliwa, kuingia Misri mwanaharakati huyo alirejea Uturuki kwa ndege nyingine. Hii ni katika hali ambayo, katika siku za hivi karibuni, serikali ya ya hivi sasa ya Misri imekuwa ikiwazuia wanaharakati wengi kuingia nchini humo.
Post a Comment