Timu zote katika ligi ya Ujerumani zinatafakari vipi zinaweza kuizuwia
Bayern Munich msimu huu. Kila timu inayokutana na Bayern inatafakari tu
jinsi ya kupunguza madhara, Schalke 04 haikuwa tofauti siku ya Jumamosi
jioni wakati ilipoingia katika uwanja wa nyumbani wa Bayern, Allianz
Arena na kujikuta ikichambuliwa kama karanga.
Baada ya kipigo cha mabao 6-1 Jumatano iliyopita dhidi ya Real Madrid ya
Uhispania katika mpambano wa Champions League, Schalke ilijikuta katika
hali ya kupimana uwezo kati ya Bayern na Real na nani anaweza kupachika
mabao mengi zaidi dhidi ya timu hiyo.
Bayern yavuna ilichopanda
Hali hiyo iliiacha Schalke ikiwa haina msaada. Bayern walikuwa wakifanya
watakavyo katika muda wote wa dakika tisini na wachezaji wa Schalke
walikuwa wakifukuza kivuli tu. Bayern walionesha mchezo wa hali ya juu
na wa kasi kupita uwezo wa wachezaji wa Schalke kama anavyosema
mshambuliaji wa Bayern Munich Arjen Robben ambaye alipachika mabao 3
jioni hiyo.
"Sifa zote zikiendee kikosi kizima cha Bayern. Tulicheza kwa kasi ya
hali ya juu, na tulifanya vizuri sana. Hatukuwaruhusu Schalke kucheza
kama wanavyotaka. Tulicheza kwa kasi kubwa, na kupachika mabao mengi.
Hiki kilikuwa kipindi cha kwanza kizuri kwetu ambacho nimewahi
kushuhudia."
Bayern sasa imekwenda michezo 20 ya nyumbani bila kufungwa ,na kushinda michezo 48 ya Bundesliga katika misimu miwili .
Katika msimamo wa ligi Bayern sasa imeweka pengo la points 20 kutoka
timu inayoifuatia ambayo ni makamu bingwa wa msimu uliopita Borussia
Dortmund ambayo ilipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya FC Nuremberg siku
ya Jumamosi.
Bayer Leverkusen katika mzozo
Bayer Leverkusen iliyokuwa inashikilia nafasi ya pili imekumbwa na mkosi
wa kukubali vipigo, baada ya wiki hii kusalim amri mbele ya Mainz 05
kwa bao 1-0. Kipigo hicho hata hivyo ni cha tano mfululizo, kipigo
ambacho kimefungua majadiliano iwapo timu hiyo iendelee kupata mafunzo
kutoka kwa kocha wake Sami Hyypiä.
Mkurugenzi wa spoti wa Leverkusen Rudi Voller amesema timu yake imepungukiwa hali ya wepesi wa kufanya mambo uwanjani.
"Kwa sasa tunakosa kabisa ile hali ya wepesi wa kufanya mambo ambayo
yanahitajika uwanjani. Hali hiyo tulikuwa nayo wakati fulani, lakini
sasa haipo kabisa. Na hiyo ndio sababu ya msingi. Na ndio sababu
hatuwezi kubadilisha lolote."
Baada ya kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Hamburg SV wiki iliyopita
Dortmund ilibidi kufanya kweli dhidi ya FC Nuremberg timu ambayo katika
mzunguko huu wa pili wa ligi ya Ujerumani wamekuwa wakifanya vizuri
ambapo wamefungwa mara mbili tu, na Bayern Munich pamoja na Borussia
Dortmund. Kocha wa Dortmund Jurgen Klopp amezungumzia ushindi huo.
"Kwangu mimi, ni siku saba tu baada ya kuwepo kule Hamburg ambapo hali
ya kufanya mambo kiurahisi uwanjani haikuonekana kabisa. Ukitaka kufanya
kazi kwa urahisi ni lazima kuwapo na wakati wa kufanyakazi kwa wepesi.
Lakini leo tumeweza kutekeleza kazi ngumu iliyotukabili."
Mpambano kati ya timu zinazowania kujitoa kutoka katika nafasi ya
kushuka daraja kati ya Eintracht Frankfurt dhidi ya VFB Stuttgart
ulimalizika kwa Frankfurt kupata ushindi wa mabao 2-1 licha ya Stuttgart
kupata bao la kuongoza ambalo lilidumu hadi katika dakika ya 80 ya
mchezo ambapo Jan Rosenthal alipachika bao la kusawazisha na dakika tisa
baadaye Alexander Meier aliwalaza mapema Stuttgart.
Mvua ya magoli
Mvua ya magoli pia ilinyesha jana huko Hoffenheim wakati timu hiyo ilipoikaribisha nyumbani Wolfsburg na kuibugiza mabao 6-2.
Ulikuwa mchezo ambao mashabiki na wachezaji wa Wolfsburg wangependa kuusahau kabisa.
Wakati huo huo kocha wa eintracht Frankfurt Armin Veh ameamua kuwa
hataifunza tena timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika, amesema
mwenyekiti wa klabu hiyo kongwe Heribert Bruchhagen leo(03.03.2014).
Amefanya kazi nzuri sana katika klabu hii kwa muda wa miaka mitatu.
Tumejaribu kumshawishi kurefusha mkataba wake lakini hatukufanikiwa,
ameongeza Bruchhagen wakati akizungumza na shirika la habari la DPA.
Pellegrini anyakua taji la kwanza
Wakati huo huo huko nchini Uingereza, baada ya kushuhudia ukame wa
mafanikio kabla ya kuingia kwa fedha kutoka kwa tajiri kutoka Abu Dhabi
mwaka 2008 , Manchester City imefanikiwa kupata taji lake la tatu ndani
ya muda wa miaka mitatu jana Jumapili, baada ya timu hiyo kunyakua taji
la kombe la ligi katika mchezo wa fainali dhidi ya Sunderland katika
uwanja wa Wembley.
Pamoja na mchezo huo wa fainali lakini pia kulikuwa na michezo mitatu ya
ligi ya Uingereza Premier League. Roberto Soldado alifunga bao lake la
kwanza katika muda wa miezi miwili wakati Tottenham Hot Spurs iliyoko
katika nafasi ya tano ya msimamo wa ligi ilipoishinda Cardiff kwa bao
1-0.
Aston Villa imejisogeza juu zaidi kutoka katika eneo la hatari ya
kushuka daraja kwa kuishinda Norwich City kwa mabao 4-1. Norwich iko
katika nafasi ya 15 katika nafasi kati ya Swansea City na Crystal
Palace, timu ambazo zilitoshana sare ya bao 1-1.
Cristiano Ronaldo aliweka wavuni bao la kusawazisha wakati Real Madrid
ikiepuka kipigo katika mchezo wa watani wa jadi dhidi ya mahasimu wao
wakubwa Atletico Madrid na kumaliza mchezo huo kwa sare ya mabao 2-2
jana Jumapili.
Barcelona ilipunguza mwanya wa points kati yake na Real Madrid hadi
point moja baada ya ushindi mnono jana wa mabao 4-1 dhidi ya vijana
machachari wa Almeria ambao wako katika nafasi ya kushuka daraja msimu
huu.
Huko nchini Italia Juventus Turin ilidhihirisha ubabe wake katika ligi
hiyo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya AC Milan na kujisogeza points 11
mbele ya timu inayoifuatilia ya Roma. SSC Napoli iliyoko katika nafasi
ya tatu ilikwenda sare ya bao 1-1 na Livorno.
Huko Ufaransa Paris St. German imeongeza uongozi wake dhidi ya Monaco
katika msimamo wa ligi ya nchi hiyo hadi points nane baada ya ushindi wa
mabao 2-0 dhidi ya Marseille.
Salomon Kalou alipachika mabao matatu wakati Lille ikiendelea
kung'ang'ania katika nafasi ya tatu kwa ushindi wa mabo 3-2 dhidi ya
Ajaccio.
Yanga na timu za Waarabu
Katika bara la Afrika Dar Young Africans ya Tanzania ilifanikiwa kwa
mara ya kwanza kuuangusha mbuyu, baada ya timu hiyo kuishinda Al Ahly ya
Misri kwa bao 1-0 nyumbani mjini Dar Es Salaam katika mchezo wa
Champions League katika bara la Afrika.
Gor Mahia ya Kenya ikapata kipigo nyumbani cha mabao 3-2 dhidi ya
mabingwa watetezi Esperance kutoka Tunisia , na Astres ya mjini Duala
Cameroon ikatoka sare ya bao 1-1 na TP Mazembe ya DRC.
Flambeau I'Est ya Burundi ikaiangusha Coton Sport ya Cameroon kwa bao
1-0 nyumbani , na Entente Setif ya Algeria ikaibugiza ASFA Yennenga ya
Burundi kwa mabao 5-0. Stade Malien ya Mali ikatoka sare ya bila
kufungana na Al-Hilal ya Sudan.
Nkana Red Devils ya Zambia ilitoka sare na Kampala City Coucil kwa kufungana mabao 2-2 mjini Ndola.
Pistorius kizimbani
Wakati huo huo kesi ya mauaji dhidi ya mwanariadha maarufu nchini Afrika
kusini anayekimbia kwa miguu ya bandia ya chuma Oscar Pistorius imeanza
rasmi mjini Pretoria.
Waendesha mashtaka wamemshitaki mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 27
kwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp na kudai yalikuwa ni mauaji ya
kukusudia.
Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo ametoa ushahidi leo kwamba alisikia
kilio kabla ya kusikia milio minne ya bunduki usiku ambapo mwanariadha
huyo alimuua mpenzi wake.
Mvuto mkubwa kwa umma wa Afrika kusini katika kesi hiyo umeoneshwa
kuzinduliwa jana usiku kwa televisheni itakayoonekana kwa saa 24 na
ambayo itakuwa inaonesha zaidi kesi hiyo mahakamani.
Bayern bado ni mlima mrefu katika Bundesliga
Title: Bayern bado ni mlima mrefu katika Bundesliga
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Bayern wakishangiria bao Timu zote katika ligi ya Ujerumani zinatafakari vipi zinaweza kuizuwia Bayern Munich msimu huu. Kila timu...
Post a Comment