PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Askari sita wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC wajeruhiwa katika shambulizi la guruneti
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Martin Kobler, Mkuu wa MUNUSCO nchini DRC Askari sita wa kutoka Nepal wa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Ja...

Martin Kobler, Mkuu wa MUNUSCO nchini DRC
Askari sita wa kutoka Nepal wa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) wamejeruhiwa kutokana na kushambuliwa kwa guruneti katika jimbo la Kivu Kaskazini kilomita mbili kutoka katikati ya mji wa Beni.

Miongoni mwa askari hao sita, wawili wamejeruhiwa vibaya.
Taarifa kutoka kwa mkuu wa MONUSCO Bw. Martin Kobler zinasema mashambulizi hayo hayatapunguza uungaji mkono wa tume hiyo kwa jeshi la serikali ya DRC katika mapambano na waasi wala kuathiri ahadi ya tume hiyo ya kusaidia kurejesha mamlaka ya serikali, amani na usalama nchini humo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top