Mhariri
Mtendaji wa New Habari Corporation Ltd, Absalom Kibanda akimkarbisha
Karibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye pia ni Mbunge wa
Mtama, alipotembelea Ofisi za kampini hiyo leo, Sinza jijini Dar es
Salaam
Karibu sana hapa ni ofisini kwako
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mhariri wa Habari wa gazeti la Mtanzania, Bakari Kimwanga
Wakienda ukumbini
Wakiwa katika mazungumzo
Kimwanga akinukuu dondoo za mazungumzo
Khamis Mkotya akiuliza swali
Nape akijibu swali
Mazungumzo yakiendelea
Mwani Nyangasa akiandika dondoo za mazungumzo
Nape na Hussein Bashe wakifurahia jambo katika mazungumzo
Naam hayo ndivyo yalivyo.....
Mkurugenzi wa New Habari Corporation Erasto Matasya akizungumza
Mazungumzo baada ya mazungumzo
Nape akiwa na Absalom Kibanda na Asha Muhajj
Nape akiwa na Asha Bani
Nape akiagana na Bashe kabla ya kuondoka.
NA BASHIR NKOROMO
Chama
Cha Mapinduzi (CCM), kimesema, kitampa ushirikiano mkubwa, Rais Dk.
John Magufuli, ili aweze kwa ufanisi zaidi mapambano yake dhidi ya
mafisadi na mikakati mingine ya kuinua uchumi wa Watanzania.
Kimesema,
kitampa ushirikiano huo Rais Dk. Magufuli, kwa sababu, aliyoanza
kuyafanya na atakayoyafanya baadaye katika uongozi wake wa Urais
anatekeleza yale yaliyomo katika ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020.
Hayo
yalisemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipokuwa
akijibu maswali kadhaa yaliyoulizwa na baadhi ya wahariri, aliokuwa
akizungumza nao, katika ziara aliyofanya leo, katika Kampuni ya New Habari Corporation, Sinza jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wahariri, waliohoji ni kwa nini CCM haijitokezi kumpongeza Dk.
Magufuli katika juhudi ambazo ameanza kuonyesha katika kupambana na
ufisadi ikiwemo kubana fedha za walipa kodi ambazo zingepotea bure
katika masuala yasiyo ya lazima na wakati huohuo kuanza kuwabana
wafanyabiashara wanaodaiwa kukwepa kulipa ushuru.
"Yapo mengi
tuliyoanisha katika ilani yetu ya Uchaguzi, na yote yahahusiana sana na
haya mnayoyaona yanafanywa na Rais Dk. John Magufuli, tena Ilani hii
tumeitunga hata kabla ya kumteua kugombea Urais, Sasa anachofaya ni
kuitekeleza ilani hii, isipokuwa mbinu anazotumia ni ubunifu wake na
hili hatuna tatizo nalo kama Chama maana kiongozi wa aina hii ndiye
tuliyemtaka", alisema Nape.
"Najua wapo wanaojaribu kutengeneza
magingira ya kumtaka kumtenganisha Dk. Magufuli na CCM, nawambieni Dk.
Magufuli ni zao la CCM na mwana CCM Kindakindaki, hivyo ni upotoshaji wa
hali ya juu kujaribu kuuaminisha umma kwamba anayofanya Dk. Magufuli
hayana uhusiano na maelekezo ya CCM", aliongeza Nape.
Alisema,
baada ya kutengeneza ilani yake, CCM, ilidhamiria kwamba, awamu hii ya
tano ni ya kutafsiri uchumi katika nyanja za huduma za Jamii, ikiwemo
miundomboni, maji, afya na elimu.
"Ni kutokana na lengo hili,
ndiyo sababu tukakaa kwa makini na kuhakikisha ilani hii ya sasa
tunamkabidhi mwana CCM ambaye utekelezaji wake hautakuwa wa mashaka
mashaka, Ndiyo huyo Dk. Magufuli, bila shaka sasa na ninyi ni mashahidi
mmeanza kuuona utekelezaji wake wa ilani", alisema Nape.
Akizungumzia
kuhusu Rais Dk. Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake la Mawaziri,
Nape alisema, Chama Cha Mapinduzi kimeshaunda serikali kwa kumpata Rais,
kilichobaki sasa ni kwa Rais mwenyewe kuteua watendaji wake, lakini
katika kufanya hivyo hakuna mda aliopangiwa kuanza kufanya hivyo na
hashurutishwi na Chama wala sheria.
Nape alisema, Dk. Magufuli
hachelewi kuteua Baraza la Mawaziri kwa sababu anakosa wakuwateua,
isipokuwa, anayo namna na mda ambao mwenyewe Kama Rais amejipangia, na
mda huo ukijiri wa kuamua kufanya hvyo atafanya.
"Tatizo hapa ni
kwamba mnayo kiu kubwa ya kutaka kujua nani atawateua, sasa kiu yenu
imepita kiasi, ndiyo maana mnaanza kuhoji, lakini mimi naamini Dk. Rais
Magufuli ataikata kiu yetu, wala msipate taabu ya kuhoji kila kukicha",
alisema Nape.
Nape alisema, mbali na Chama kutengeneza ilani
ambayo italeta mageuzi makubwa ya kiuchumi hapa nchini, pia Watanzania
watarajie kuona mageuzi makubwa ndani ya CCM, kwa sababu yapo njiani
kuwadia.
"Kama ilivyo kawaida yetu, kila baada ya uchaguzi mkuu
huwa tunafanya tathmini, baada ya tathmini hiyo, huwa lazima tufanye
mageuzi kwa yale ambayo tumebaini kuwa ni kikwazo kwa uhai na maendeleo
ya Chama katika nyanja mbalimbali, na mageuzi haya tunayafanya
kuzingatia mahitaji ya sasa na wakati ujao", alisema Nape.
Kuhusu
Mwenyekiti wa sasa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kumwachia Ueneyekiti
Rais Dk. Magufuli, Nape alisema, hayo si mambo mageni kwa CCM, imekuwa
ikifanyika katika awamu zote za Urais, hivyo Kikwete anaweza akaamua
kumwachia kabla ya uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika mwaka 2017 au
kabla ya hapo akiona inafaa.
Zanzibar
Akizungumzia mgogoro wa
Zanzibar uliotokana na kufutwa uchaguzi mkuu wa Rais wa Zanzibar, Nape
alikiri kamba ni mbaya na unaitia doa Tanzania, akisema, lakini
akasisitiza kwamba njia pekee ya kuumaliza ni kwa mazungumza baina ya
viongozi wa ndani bila kushirikishwa mataifa ya nje.
Alisema,
msingi wa mgogoro uliojitokeza Zanzibar, si wa kisheria, bali ni wa
kisiasa zaidi, hivyo juhudi ziwekwe kwenye mazungumzo kuutatua, na baada
ya kuutatua yaendelee kufanyika mazungumzo ambayo yataleta suluhisho la
kudumu kwa kuwa imekuwa ni kawaida kwa Zanzibar kuzuka migogoro kila
baada ya uchaguzi mkuu jambo linaloonyesha kuwa tatizo ni la asili zaidi
kuliko inavyodhaniwa.
Katika mazungumzo yake na wahariri hao wa
New Habari Corporation Ltd, Wachapishaji wa magazeti ya Rais, Mtanzania
na Dimba, alivitaka vyombo vya habari nchini, sasa kushirikiana na
Serikali kulijenga taifa.
"Tunajua wakati wa kampeni kulikuwa na
mambo mbalimbali ambayo wakati mwingine vyombo vya habari vililazimika
kukampenia vinaowaona kuwa wanafaa kutokana na sababu mbalimbali, lakini
kama tulivyokuwa tukisema, kwamba baada ya uchaguzi maisha yataendelea,
sasa umefika wakati wa kuendelea na maisha tuwe kitu kimoja", alisema
Nape.
Alivitaka vyombo vya habari, kusaidia kuishari Serikali na
CCM, katika kutekeleza yaliyo bora kwa taifa na hata pale vyombo hivyo
vitakapoona kwamba Chama au serikali vinaenda kinyume, visihofii
kukosoa.
Kwa upande wao, Mtariri Mtendaji wa Habari Corporation,
Absalom Kibanda akimpongeza Nape kwa ushirikiano ambao amekuwa akivipa
vyombo vya habari, na kumtaka aendelee kuwacha milango wazi kwa
waandishi wa habari kama ambavyo amekuwa akifanya.
Ziara hiyo ya
Nape aliyoianza jana, kwenye vyombo vya habari inatarajiwa kuendelea
kesho kwa kutembelea vyombo vingine vya habari vyenye makao yake makuu
jijini Dar es Salaam.