PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: UNDP, GEF WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAZINGIRA KWA NJIA ASILI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Mwandishi wetu,Dodoma Wakati shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia program ya miradi midogo inayodhaminiwa na Mfuko wa...

  





Mwandishi wetu,Dodoma


Wakati shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia program ya miradi midogo inayodhaminiwa na Mfuko wa Mazingira Duniani(GEF) ukieleza kuridhishwa na utekelezwaji wa miradi 24 ya mazingira nchini,wadau wa mazingira  wameitaka Serikali kuishirikisha jamii kwenye utungaji wa sera na sheria ili kurahisisha uhifadhi endelevu wa raslimali asili.


Wakizungumza katika kikao cha kujadili matokeo ya miradi iliyofadhiliwa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP), chini ya Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) Kamati ya kitaifa ya Usimamizi wa miradi hiyo na waliotekeleza  miradi wote kwa pamoja walikubaliana umuhimu wa kuendelezwa miradi  hiyo.



Miradi hiyo 24, ni ile ambayo ni kipaumbele kwa jamii ambayo inahusu masuala ya ardhi, uendelezaji wa maeneo ya malisho, uhifadhi wa misitu na vyanzo vya maji, utunzaji wa mazingira


Akifungua mkutano huo,Mwenyekiti wa Kamati ya Uendeshaji ya GEF Small Grants Programme Dkt. Damas Mapunda, alieleza kuridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo .


Dkt. Mapunda ambaye anatoka Ofisi ya Makamu wa Rais alisema serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa mazingira kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kuhifadhiwa.


"Tumesikia taarifa za miradi yote kwa ujumla kazi nzuri infanyika na sisi kama Kamati na serikali bado tutaendelea kushirikiana katika masuala ya uhifadhi mazingira,vyanzo vya Maji na Misitu "alisema 


Mratibu wa Programu ya Ruzuku Ndogo za GEF kupitia shirika la UNDP, Faustine Ninga alisema katika kipindi cha miaka miwili tangu mwaka 2021, wamekuwa na miradi 24 ambayo imetekelezwa kwenye maeneo mbalimbali nchini na kukamilika Juni mwaka huu kwa mafanikio.


“Leo hii tumekutana ili kushirikishana matokeo ambayo tumeyaona kwenye miradi hii, changamoto na mambo ambayo tunaweza kujifunza kupitia utekelezaji wa miradi hii sasa na ujumbe gani wa kisera uliopatikana kupitia miradi hii,”alisema.


Alisema miradi hiyo ilikuwa na thamani ya Sh1.5 bilioni (sawa na Dola za Marekani Milioni Moja), ilifadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF), uliopo chini ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP).


Alisema wanufaika wa miradi hiyo, wanatoka katika jamii kutoka mikoa ya Arusha, Simiyu, Morogoro, Mara, Manyara na Ruvuma.


Ninga alitaja changamoto walizoziona wakati wa utekelezaji wa mradi huo ni uhitaji mkubwa wa ruzuku katika kutekeleza miradi ya jamii kwasababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, ujangili uhifadhi wa mazingira.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF), Zakaria Faustine alisema lengo la kukutana ni kushirikishana matokeo yaliyotokana na namna gani ya kutumia maarifa ya asili kusimamia vyanzo vya maji, malisho misitu na wanyamapori na maeneo yenye ikolojia ya Tanzania.


“Tumejaribu kushirikisha Serikali kuja kuona ni namna gani ya kutumia njia mbalimbali za kutumia, kutunza na kuendeleza maliasili za asili ili wakati wa maboresho ya sera na sheria waweze kutambua namna gani ya kumshirikisha mwananchi kusimamia raslimali zake,”alisema.


Faustine alishauri jamii ziendelee na njia zao za kukuza raslimali za asili kwa ajili ya kizazi kilichopo na kijacho.

Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la (MIMUTIE WOMEN ORGANIZATION), Rose Njilo aliwataka watunga sera kuhakikisha kuwa wanawashirikisha wananchi ili waweze kujumuisha mawazo ya wanaotumia sera.


“Tumekuja kwa pamoja jamii za pembezoni ambazo ni jamii za kifugaji, wakulima na waokota matunda. Miradi hii imemgusa mwanamke moja kwa moja kwa kuwa ni miradi inayoshughulika na maji na malisho,”alisema.


Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi,Profesa Hezron Nonga akizungumza katika mkutano huo, alipongeza miradi hiyo kutokana na kugusa suala la malisho ya mifugo ambayo ni changamoto kubwa kwa sasa nchini.


"Nimesikiliza miradi mingi naona imegusa suala la malisho ya mifugo ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi ni jambo jema na sisi kama Wizara tutashirikiana kuhakikisha mbegu za malisho zinawafikia wafugaji"alisema.


Wajumbe wengine wa Kamati ya kitaifa ya Usimamizi wa miradi ya GEF pia walipongeza miradi kwa kugusa makundi yote katika Jamii wakiwepo wanawake,vijana na wazee katika utekelezwaji wa miradi katika Jamii.


Hata hivyo walitaka miradi hiyo iwe endelevu kwa kuhakikisha Jamii inashirikishwa ili matunda yake yaendelee kuonekana kwa muda mrefu.




About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top