PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: CHEMCHEM ASSOCIATION KUTUMIA BILION 1.5 KUDHIBITI UJANGILI ENEO LA BURUNGE WMA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Meneja wa Chem chem foundation Clever Zulu akimkabidhi kamanda wa Polisi Mkoa Manyara George Katabazi, luninga ya kisasa kwa ajili ya kufu...

 

Meneja wa Chem chem foundation Clever Zulu akimkabidhi kamanda wa Polisi Mkoa Manyara George Katabazi, luninga ya kisasa kwa ajili ya kufuatilia matukio mbalimbali katika  eneo la Burunge WMA na Mfumo Ikolojia Manyara Tarangire.

 
Afisa wa TAWA Emmanuel Pius akizungumza Katika mafunzo ya kuwajengea uwezo Askari was wanyamapori eneo la Burunge WMA

Mwendesha mashitaka wa TAWA, Getrude Kariongo akitoa mafunzo Askari wa Burunge WMA


Mwandishi wetu, Babati 



Taasisi  ya chem chem foundation imetenga zaidi ya bilioni 1.5 katika  kuendeleza uhifadhi na kupambana na ujangili  mwaka wa fedha 2023/24 katika eneo la Jumuiya ya Hifadhi   Wanyamapori ya Burunge,wilayani Babati mkoa wa Manyara.

Mkakati huo wa uhifadhi, unashirikisha Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Burunge WMA, Halmashauri ya wilaya ya Babati na Taasisi ya Chemchem association ambayo imewekeza katika eneo hilo.

 Meneja wa chemchem association, Clever Zulu alisema , Chemchem association imeamua kuongeza bajeti ili kuhifadhiwa kwa eneo hilo muhimu Katika ikolojia ya Tarangire na Manyara.


“Tulikuwa na bajeti ya shilingi 500 milioni lakini sasa tumeongeza hadi kufikia dola 700,000 ambazo ni zaidi ya bilioni 1.5 lengo ni kuhifadhi eneo hili ili kuvutia watalii zaidi”amesema

Alisema katika eneo hilo wamekuwa wakifanya utalii w.a picha  na hoteli za kitalii na watalii wameendelea kuongezeka kutokana na jitihada za uhifadhi ambazo zinafanywa.

Eneo la Burunge WMA, lipo kati kati ya hifadhi ya Taifa ya Tarangire na Hifadhi ya Manyara, likiwa na ukubwa wa kilomita za mraba 283 likiundwa na vijiji 10 ambavyo ni  mwada, vilima vitatu, Sangaiwe, Ngolei,Minjingu,Kakoi,Olasiti,Magara,Maweni na  kijiji cha Manyara.


Afisa Mhifadhi wa TAWA Kanda ya kaskazini,  Emmanuel Pius amesema mpango wa uhifadhi eneo hilo unatarajiwa kuwa shirikishi na kushirikisha wadau wote wakiwepo wananchi.


“Tunataka eneo hili kuwa la mfano katika uhifadhi, tumetoa mafunzo kwa askari wa wanyamapori, kuna vikao vya kueleza umuhimu wa uhifadhi ambavyo vitashirikisha wazee wa mila na wazee maarufu wa eneo hili na kuna vikao vya vyombo vya ulinzi na usalama”alisema

Katibu wa Burunge WMA, Benson Mwaise alisema kutokana na jitihada za uhifadhi kuwa nzuri katika eneo hilo,  watalii ambao wanatembelea kujionea vivutio , wamekuwa wakiongezeka  sambamba na mapato.

Mkazi wa Kijiji Cha vilima vitatu, Julius Maliaki alipongeza Taasisi ya chem chem kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya uhifadhi .

" Hili eneo kabla ya huyu mwekezaji chemchem kulikuwa hakuna  wanyamapori wengi na Mazingira yalikuwa yameharibika Sana lakini Sasa limetunzwa vizuri na Kuna wanyamapori wengi na ujangili umedhibitiwa Sana"amesema.





About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top