Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameridhia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ulioandaliwa na Baraza la Wanawake la chama hicho (Bawacha) itakayofanyika Machi 8 mwaka huu mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Machi 5, 2023 katika hotel ya corridor spring Jijini Arusha, Mbowe amesema kuridhia kwa Rais Samia kumetokana na mwaliko waliompa siku chache zilizopita.
“Nikitambua namna ambavyo tumefanya kazi na Rais Samia tumekubali tumualike na yeye amekubali kuhudhuria aje awasikie wakinamama wa Chadema, kina mama wa upinzani.
Siku zote anawasikiliza wakina mama wa chama chake, aje awaone atambue kazi kubwa inayofanywa na akina mama wa Chadema kwa hiyo Rais atakuwa mgeni rasmi katika tukio letu na mimi nitakuwepo kumpokea,” amesema Mbowe.
Amesema katika mkutano huo si Rais Samia pekee, wanawake wenye itikadi mbalimbali za kisiasa wamealikwa kwa kile alichokifafanua kuwa maadhimisho hayo si ya Chadema bali ya wanawake wote duniani.
Post a Comment