PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Lema Amuomba Rais Kuruhusu Biashara ya Madini ya Tanzanite Kufanyika Jijini Arusha
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
GODBLESS LEMA akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo    Na: Onesmo Mbise Arusha  Mwenyekiti  Chadema Kanda Ya Kaskazini Godbless Lema...

GODBLESS LEMA akizungumza na Waandishi wa Habari mapema leo 


 

Na: Onesmo Mbise Arusha 


Mwenyekiti  Chadema Kanda Ya Kaskazini Godbless Lema Ametoa Kwa  Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani Kuondoa Marufuku ya kutokuuza Madini Ya Tanzanite nje ya Mji Wa Mererani kwani Kufanya Hvyo ni kulifanya Soko la Tanzanite Kuzorota  Hapa Nchini.


Lema Amesema  hayo katika Mkutano wake na vyombo vya Habari Jijini Arusha  ambapo Ameeleza Kuwa  Kuuza Madini ya Tanzanite Katika Mjii wa Mererani Pekee ni   kosa la Kimkakati la Kibiashara ambalo Linayafanya Madini ya Tanzanite yasiwe na thamani Kwa Watanzania.


Amesema kuwa  ni wakati Sasa Serikali  Kuruhusu Mfumo wa Biashara Kwa  Madini Hayo kuwa Katika Soko Huria Ili  Madini yapatikane Kwa wepesi Ndani na nje ya Nchi na Kwa kufanya Hvyo kutaongeza Soko na Uhitajio Wa Madini Hayo.


Aidha Ameitaka Serikali Kuangalia Namna Ya kuweka Mfumo wa kielectronikia  utakao Saidia  Kutambua Uhalali  Madini ya Tanzanite Sokoni  Ili kuepusha wizi au utoroshaji unaoweza kufanyika kiholela.


Lema Amebainisha Kuwa Mfumo wa Soko Huria katika Uuzaji wa Madini ya Tanzanite Utaongeza Mapato ya Serikali na hvyo kuchangia Ukuaji wa Uchumi wa Nchi ya Tanzania.


Pia Lema Amesema kuwa  Arusha Ni Jiji la kitalii hvyo Serikali inapaswa Kuruhusu Biashara hyo Kufanyika Arusha mjini kupitia Broka ambao Wana leseni za Kufanya Biashara hyo Ili kuwezeshaji upatikanaji wake kwa wepesi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top