PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MOTO WATEKETEZA BWENI LA SEKONDARI YA LUGARAWA WILAYANI LUDEWA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
 Na. Damian Kunambi, Njombe. Moto ambao chanzo chake kikihisiwa kuwa ni hitilafu ya umeme umeteketeza bweni la wavulana katika shule ya se...

 Na. Damian Kunambi, Njombe.

Moto ambao chanzo chake kikihisiwa kuwa ni hitilafu ya umeme umeteketeza bweni la wavulana katika shule ya sekondari Lugarawa iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe na kuunguza vitu mbalimbali ikiwemo vitanda, magodoro na baadhi ya vifaa vingine vya wanafunzi ambavyo kwa ujumla pamoja na jengo vimekadiliwa kuwa na thamani ya zaidi Tsh. Ml. 18.

Akizungumza mara baada ya kuwasili viongozi mbalimbali wa halmashauri ya wilaya hiyo sambamba na kamati ya ulinzi na usalama, mkuu wa shule hiyo Everine Somola amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tatu usiku wakati wanafunzi wakiwa darasani kwa masomo ya usiku.

"Bweni hili wanaishi wanafunzi 82 na wakati moto huo unatokea hakukuwa na mwanafunzi bwenini isipokuwa huwa tuna utaratibu wa kila baada ya lisaa limoja wanafunzi wawili huzungukia mabweni kuangalia usalama hivyo muda huo wanafunzi walipita na kuona moto huo ukiwaka kwenye main switch huku moshi ukiwa umetanda eneo lote".

Aidha kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Castory Kibasa amesema tayari hatua za awali zimeanza kuchukuliwa kwa kununua magodoro na vitu vingine lakini bado wanahitaji msaada zaidi kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuhakikisha mazingira ya wanafunzi hao yanarejea katika hali ya kawaida.

Sanjari na hilo pia amemshukuru mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kwa kuonesha ushiriki wa haraka ambapo baada ya kupata taarifa ametoa kiasi cha sh. Milioni moja na kuahidi kufika eneo hilo hivi karibuni.


Deogratias Massawe ni mkuu wa polisi wilaya ya Ludewa amewataka walimu na viongozi wa shule zenye mabweni kuhakikisha wanafuata utaratibu wa ulinzi waliofundishwa na askari ambao wamekuwa wakipita mashuleni kwa lengo la kutoa elimu mbalimbali za usalama.

" Tumekuwa tukipita katika shule mbalimbali na hasa ambazo wanafunzi wanaishi hapo, na kuwapa elimu juu ya ulinzi shirikishi ambapo muda wa masomo ya usiku wanatakiwa kuwepo bwenini wanafunzi watano kwaajili ya kulinda usalama pia viwepo vifaa vya kuzimia moto kama ndoo zilizojazwa mchanga", amesema Afande Masewe.








About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top