PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAMLAKA UVUVI BAHARI KUU KUJENGA KIWANDA CHA KUCHAKATA SAMAKI JIJINI TANGA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mkurugenzi wa Mamlaka ya kusimamaia uvuvi na Bahari kuu Tanzania Emanuel Sweke akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya ...

Mkurugenzi wa Mamlaka ya kusimamaia uvuvi na Bahari kuu Tanzania Emanuel Sweke akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma


Wandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu wa usimamizi wa uvuvi wa Bahari kuu Tanzania pichani hayupo

NA: SHAKILA NYERERE, DODOMA

maipacarusha20@gmail.com


 MAMLAKA ya kusimamia uvuvi wa Bahari Kuu imesema kuwa katika kutekeleza mikakati yake inatarajia Kujenga Kiwanda kikubwa Cha kuchakata Samaki Mkoani Tanga ambacho kitakuwa na uwezo wakuzalisha Tani zaidi ya 100 kwa siku ambacho kitagharimu Dola Milioni10 na kutoa fursa ya ajira kwa Watanzania.


Hayo ameyasema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo,Dk Emanuel Sweke wakati akizungumza na waandishi wa habari hayo Jijini Dodoma kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka ya usimamizi wa Bahari Kuu mbele ya Waandishi wa Habari.


Aidha amesema kuwa katika kudhibiti uvuvi haramu Mamlaka hiyo imeweza kuweka mifumo madhubuti ambayo inaendana na Teknolojia kwakufanya doria mbalimbali kwajili ya kukomesha suala la uvuvi haramu.

Pia amesema kuwa kutokana na shughuli zake Mamlaka hiyo imeweza kuvunja rekodi ya kukusanya Mapato mengi kwa Kipindi Cha 2022 hadi kufikia Shilingi Bilioni4.1 huku akisema hadi Sasa wametoa jumla ya leseni za uvuvi 5336.

Mamlaka ya kusimamia uvuvi wa Bahari Kuu imeanzishwa rasmi Mwaka 2010 lengo lake likiwa ni kusimamia shughuli zote za uvuvi wa Bahari Kuu na ufuatiliaji.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top