MLIMA KILIMANJARO |
Na: Mwandishi wetu, Arusha
Makamu wa Rais dkt Philip Mpango anatarajiwa kushuhudia hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ikitimiza miaka hamsini tangu kuanzishwa kwake march 16 Mwaka huu.
Naibu Kamishna wa Uhifadhi na maendeleo ya biashara,Herman Batiho aneyasema hayo alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari makao makuu ya hifadhi za Taifa TANAPA Jijini Arusha mapema Leo.
"Kilele cha Mlima kilimanjaro kitafanyika Marangu Mkoani Kilimanjaro yalipo makao makuu ya Mlima huo huku makamu wa rais dkt Philip Mpango akitarajiwa kuwa mgeni rasmi " Alisema
Maadhimisho hayo yatakayohusisha usafi wa Mlima utakaofanyika kwa siku kumi kuanzia machi 1,ambapo wadau wa utalii wapatao 500 watashiriki.
Amesema kuwa Shughuli zingine zitakazofanyika katika sherehe za maadhimisho hayo ni pamoja na ugawaji na upandaji wa miti, zoezi litakalozinduliwa na mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu.
"Pia tutawatembelea waongoza utalii wa miaka ya 70 ili kuzungumza nao na kupata uzoefu wao na ushauri wao"
Alisema tangu kuanzishwa kwa shughuli za utalii katika mlima Kilimanjaro, mafanikio kadhaa yamepatikana ikiwemo ongezeko la watalii na kufikia elfu 50 kwa mwaka, kuongezeka kwa njia za kupandisha mlima huo kutoka njia moja hadi kufikia njia sita
Post a Comment