PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAIPAC WASAMBAZA VITABU KWA MAKUNDI MAALUM NA WANAFUNZI WILAYANI LONGIDO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Wanafunzi wa shule ya Msingi Orbomba wilayani Longido wakifurahia vitabu VYA MAARIFA YA ASILI KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA walivyogaiwa ...

  

Wanafunzi wa shule ya Msingi Orbomba wilayani Longido wakifurahia vitabu VYA MAARIFA YA ASILI KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA walivyogaiwa na Maipac

Mkurugenzi wa Maipac Mussa Juma akigawa baadhi ya vitabu kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Orbomba

Baadhi ya wakina Mama wa jamii ya Kimasai wakisoma na kufurahia KITABU CHA MAARIFA YA ASILI KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA


Mwandishi wetu Maipac, Longido 

maipacarusha20@gmail.com


Shirika la wanahabari la kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) limeanza kusambaza vitabu vya maarifa ya asili katika utunzaji wa Mazingira, misitu na Vyanzo vya maji, katika makundi mbalimbali ikiwepo mashuleni,kwa vijana na makundi mengine.

Vitabu hivyo,vilizinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dr Seleman Jafo jijini Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita.

Vitabu hivyo, ambavyo vinatokana na simulizi la viongozi wa Mila ya kimasai, wanawake na vijana vimechapishwa Ikiwa ni sehemu ya mradi wa Uhifadhi na utunzwaji Mazingira kwa maarifa ya Asili ambao unaofadhiliwa na mfuko wa Mazingira duniani (GEF) kupitia shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) katika program ya miradi midogo.

Vitabu 3000 vinatarajiwa kusambazwa katika wilaya za Longido,Monduli na Longido lakini pia katika taasisi mbalimbali za serikali na binafsi ndani na nje ya nchi.

Akizindua vitabu hivyo,Waziri Dk Jafu alisema vitakuwa na Msaada mkubwa kwani jamii kwa Sasa imeanza kusahau maarifa ya asili katika. mambo mbalimbali ya kijamii ikiwepo utunzwaji wa Mazingira.

Dk Jafo alisema kitabu hicho,kitapelekwa kwa wataalam wengine Ili kuona kinaweza kutumika zaidi katika eneo lipi.

Hata hivyo, Waziri  Dk Jafo alipongeza mfuko wa Mazingira dunian ( GEF) na UNDP kusaidia mashirika madogo katika miradi ya utunzaji Mazingira ambayo Inaguza  Moja Kwa Moja Wananchi.

"Nawaomba UNDP na GEF kuendelea kusaidia MAIPAC ma wengine katika miradi hii kwani hali ya uhalibufu Mazingira ni mbaya Dunia na jitihada kubwa zinahitajika kwa kushirikiana wadau mbalimbali "alisema


Mratibu wa program  ya midogo ya Mazingira kupitia GEF ambayo inasimamiwa  na shirika la UNDP , Faustine Ninga alisema vitabu hivyo vitasaidia kurithisha maarifa ya asili kutoka vizazi vya Sasa na vijavyo.

Afisa Utawala Maipac Andrea Ngobole kulia akimkabidhi kitabu bi Ngisho Iyare wa Kijiji Cha Oritepesi kata ya Orbomba wilayani Longido


Afisa Utawala wa MAIPAC Andrea Ngobole amesema shirika la MAIPAC wa kushirikiana na shirika la CILAO pia wametengeneza makala ndefu na fupi za video za maarifa ya asili ambazo zitaendea kusambaza kwenye vyombo vya habari .


"Vitabu hivi tunatarajia vitasomwa na Wanafunzi,vijana , wanawake na makundi mengine katika jamii ikiwepo watungaji wa sera Ili kusaidia kutunzwa Mazingira "amesema


Wakizungumza baada ya kupokea vitabu mwalimu wa shule ya msingi Olbomba Lekishoni Mollel alipongeza MAIPAC Kwa kusambaza vitabu.


"Vitabu hivi nimesoma kidogo ni vizuri na tutawapa vijana wawe wanajisomea haya maarifa ya asili katika uhifadhi wa Mazingira"alisema

Diwani wa kata ya Orbomba Ndiono Mollel katikati akipokea kitabu Toka kwa Mkurugenzi wa Maipac Mussa Juma na kulia ni mwenyekiti wa Kijiji Cha Orbomba alifurahia kitabu hicho


Diwani wa Kata ya Olbomba Ndiono Mollel pia Akizungumza baada ya kupokea vitabu hivyo,alipongeza MAIPAC kurejesha vijijini vitabu hivyo.


"Vitabu hivi ni muhimu sana kwani wilaya yetu ya Monduli imeathirika sana na mabadiliko ya tabianchi hivyo wanafunzi na vijana wakisoma vitasaidia kutunza Mazingira "amesema.


Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa Arusha,Blandina Nkini alipongeza pia MAIPAC kuwa na mradi wa kipekee wa Uhifadhi Mazingira kwa maarifa ya asili na kueleza anajivunia shirika hilo pekee kati ya mashirika 1114 mkoa Arusha linalofanya kazi nzuri ya kuhimiza utunzwaji Mazingira kwa maarifa ya asili.


Mradi huu wa maarifa ya asili katika uhifadhi pia umeshirikisha maarifa wa  Halmashauri za Monduli, Longido na Ngorongoro katika hatua zote ikiwepo uhakiki wa taarifa za maarifa ya asili .




About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top