PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Shirika la CORDS latoa msaada wa Mahindi Kaya 395 zinazokabiliwa na njaa Longido
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Afisa miradi wa CORDS Martha Katau akizungumza na wakazi hao kabla ya kukabidhi mahindi kwa baadhi wananchi Longido. Afisa miradi wa CORD...

 

Afisa miradi wa CORDS Martha Katau akizungumza na wakazi hao kabla ya kukabidhi mahindi kwa baadhi wananchi Longido.

Afisa miradi wa CORDS Martha Katau akikabidhi mahindi  kwa baadhi wananchi Longido.



Na: mwandishi wetu, Longido


Shirika la Utafiti, Maendeleo na Huduma kwa jamii( CORDS) jana limekabidhi  tani 7.1 za mahindi kwa kaya 395 za vijiji viwili  vya wilaya ya Longido mkoa wa Arusha ili kukabiliana na uhaba wa chakula.


Akizungumza wakati wa ugawaji mahindi hayo, ,Afisa miradi wa shirika la CORDS , Martha Katau alisema wameamua kutoa mahindi ya msaada baada ya kubaini kaya nyingi zinakabiliwa na njaa.


"tumekuwa na miradi kadhaa hapa Longido, ikiwepo ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, lakini tumebaini kuna upungufu wa chakula kwa kaya nyingi na hivyo tumeona tusaidie walau kidogo"alisema

Ugawaji wa mahindi ukiendelea kwa wakazi wa Longido



Alisema katika mgao huo, kijiji cha  Ildonyo kaya 165 zimepatiwa tani 2.6 na kijiji cha Orpurkel Kaya 230 zimepatiwa tani 4.5 ili kusaidia kukabiliana na upungufu wa chakula.

Kaimu Afisa kilimo wa wilaya ya Longido, Mariam Fivawo  alisema  ukame umesabisha uhaba wa chakula katika maeneo mengi ya wilaya hiyo ambayo asilimia 95 ya wananchi ni wafugaji.

Hata hivyo, aliwataka wananchi wenye mifugo kujitahidi kuuza baadhi ya mifugo yao  ili waweze kununua chakula cha bei nafuu ambacho tayari kimepelekwa na serikali katika wilaya hiyo.


Viongozi wa CORDS wakiiimba na kufurahi pamoja na wanufaika wa msaada wa mahindi hayo


Moja ya wakazi waliopatiwa msaada wa CHAKULA akiwa anaelekea nyumbani kwake


Mmoja wa wanufaika wa msaada huo, Witness Alais  alisema msaada huo wa mahindi utasaidia sana kukabiliana na njaa kwani licha ya kukosa chakula lakini pia hata maziwa ya mifugo hawana kutokana na mifugo mingi kufa kwa ukame na iliyobaki haiwezi kuzalisha maziwa kwa wingi.

"tunashukuru shirika la CORDS kwa kutupa msaada huu ambao  utasaidia hasa akina mama na watoto ambao wanashida kubwa zaidi ya chakula"alisema


Shirika hilo pia wiki iliyopita lilitoa msaada wa mahindi  tani 12  kwa kaya 553 katika  vijiji vya Idonyonaado  na Emuruwa  katika kata ya Mfereji wilaya ya Monduli  mkoa Arusha.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top