PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: CORDS WATOA MSAADA WA TANI 12 ZA CHAKULA KWA KAYA ZENYE NJAA WILAYANI MONDULI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Pichani ni wakazi wa Monduli wakisubiri kugaiwa MSAADA WA chakula na SHIRIKA LA cords   Ugawaji wa chakula Cha mahindi ukiendelea NA: mwandi...

Pichani ni wakazi wa Monduli wakisubiri kugaiwa MSAADA WA chakula na SHIRIKA LA cords

 
Ugawaji wa chakula Cha mahindi ukiendelea




NA: mwandishi wetu, Monduli

  Shirika la Utafiti, Maendeleo na Huduma kwa Jamii( CORDS ) limetoa msaada tani 12 za mahindi ya bure kwa kaya 553 za wilaya ya Monduli mkoa Arusha, ili kukabiliana na njaa .

msaada huo umetolewa kutokana na wakazi wengi wa Monduli kukabiliwa na njaa.

Afisa Miradi wa   CORDS Martha Katua  amesema shirika hilo limetoa msaada huo baada ya kubaini Kaya nyingi kukabiliwa na uhaba wa chakula

Katau amesema wamegawa Tani 12 za Mahindi kwa kaya 553 katika Kata ya Mfereji Wilaya ya Monduli.

Amesema  vijiji ambavyo vimenufaika na msaada huo ni Kijiji Indonyonaado ambacho kimepatiwa Tani 6.5 kwa kugawanywa kwa Kaya 301 na Kijiji cha  Emuruwa jumla ya Kaya 252  zimepata Tani 5.5 za Mahindi.

Mmama akiwa anafunga Debe lake la mahindi alilogaiwa na cords



Mwenyekiti wa Bodi ya CORDs Yohana Ordorop alisema jamii ya wafugaji Monduli inakabiliwa na njaa kutokana na ukame.

"wafugaji wanategemea kuuza mifugo ili wanunuwe chakula ila sasa ukame umeua mifugo na mingine kukonda"alisema



Kaimu Afisa Kilimo , wilaya ya Monduli Theobald Ngobya amesema wilaya hiyo inahitaji tani 28,000  za chakula.

Ngobya alisema kumekuwepo na uzalishaji mdogo wa chakula kwa misimu zaidi ya miwili mfululizo katika wilaya hiyo hatua ambayo imesababisha upungufu wa chakula.

Amesema wilaya hiyo inaupungufu wa mahindi Tani 22,550 na maharage Tani 7578 ili kupunguza tatizo la uhaba wa chakula katika maeneo mengi.

Jeremiah John  amewapongeza CORDS kwa kuwapa msaada wa chakula kwani wanauhaba wa chakula.

John ameomba mashirika mengine  na serikali kuwasaidia.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top