PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MASHIRIKA YASIYO YA SERIKALI YATOA TAMKO UTAIFISHWAJI MIFUGO, WAOMBA KUKUTANA NA RAIS SAMIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Baadhi ya mifugo iliyopigwa MNADA hivi karibuni Na: Mwandishi wetu Serikali imeombwa kusitisha zoezi la kutaifisha mifugo ambayo inakamatw...

 

Baadhi ya mifugo iliyopigwa MNADA hivi karibuni


Na: Mwandishi wetu

Serikali imeombwa kusitisha zoezi la kutaifisha mifugo ambayo inakamatwa maeneo yaliyohifadhiwa,kwani inafilisi wafugaji nchini ambao kwa asili ndio wahifadhi wakubwa.

Wakili Alais Melau akifafanua jambo kwa wanahabari


Wakizungumza na waandishi wa habari, wakurugenzi wa mashirika 10 ambayo yanatetea haki za binaadamu na wafugaji,wameomba serikali kusitisha utaifishwaji mifugo kwani, kunawafilisi  wananchi wake ambao wanategemea mifugo kama chanzo kikuu cha kipato katika maisha yao.

Mifugo  zaidi ya 5000 imetaifishwa na serikali  na kuuzwa kwa mnada , mingine zaidi ya 2000 imekamatwa wilaya ya Simanjiro mkoa Manyara  ikisubiri kuuzwa kwa mnada wiki baada ya kuingia katika hifadhi ya taifa ya Tarangire.


Mkurugenzi Shirika la Integrated Development Initiative in Ngorongoro(IDINGO), Loseria Maoi akisoma tamko la mashirika hayo


Mkurugenzi Shirika la Integrated Development Initiative in Ngorongoro(IDINGO), Loseria Maoi alisema  wanaomba  Serikali iimarishe  ujirani mwema na wananchi wanaozunguka maeneo ya hifadhi  na kutoa elimu kwa wananchi kuepuka kutumia nguvu kwa wananchi wake na ikizingatiwa kuwepo kwa athari za mabadiliko makubwa ya tabia nchi inayosababisha ukame wa muda mrefu.

“tunaiomba sana serikali kuwafikiria wananchi wake kwani wanabaki masiki mfano Desemba 14  2022 ng’ombe 1,772 mali ya wafugaji wa Loliondo  Wilaya ya Ngorongoro katika Mkoa wa Arusha waliuzwa kwa mnada wa hadhara kwa amri ya mahakama kwa madai kuwa mifugo hiyo haina mwenyewe na kuacha kaya zaidi 22 zikiwa masikini”alisema

Mkurugenzi wa SHIRIKA LA PALISEP, Robert Kamakia akizungumza na waandishi wa habari


Mkurugenzi wa shirika la PALISEP, Robert Kamakia alisema ni muhimu serikali iache kutaifisha mifugo ya wananchi na badala yake kutengeneza mifumo rafiki inayoweza kutatua changomoto zilizopo baina ya hifadhi za taifa na wafugaji wa asili  wanaozunguka maeneo hayo.

“kwa miaka mingi hawa wafugaji ambao leo wanaonekana ndio maadui ya hifadhi na wanyamapori ndio walikuwa wanaishi na wanyama nan i maeneo yao pekee nchini ndipo kuna wanyamapori sasa lazima waangaliwe maisha yao kwa kulinda ardhi yao ya ufugaji”alisema




Alisema  mfano hao wa mgogoro wa ardhi ni sehemu kubwa ya wananchi wa vijiji 14 vinavyozunguka eneo la kilomita za mraba 1500 na eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wanakabiliwa na baa la njaa hivyo ni jukumu la serikali kuwapa misaada ya kibidamu hasa msaada wa chakula”alisema

Mkurugenzi wa shirika la ustawi wa wanawake na watoto ( WOCWELS) Mary Mushi akisoma tamko kwa niaba ya wakurugenzi wa mashirika yasiyo ya serikali.


Mkurugenzi wa shirika la kutetea wanawake na watoto (WOCWELS) Mary Mushi alisema wafugaji wanaomba viondolewe vikwazo vya kuonana na Rais, Dr. Samia Suluhu Hassan kwani wanaamini kuwa shida zao hazifikishwi  kwake na kujua adha ambayo wanapata .

“hawa ni  wapiga kura wa Rais Samia ambao kwa miaka yote wamekuwa walinzi wa hifadhi za taifa na maeneo mengine yaliyohifadhiwa lakini wapo katika adha kubwa kwa sasa “alisema

Wakili Alais Melau alisema ni muhimu sana serikali Watendaji wa serikali waheshimu maamuzi ya Mihimili mingine kama Bunge na mahakama kwani baadhi ya maeneo ambayo mifugo imetaifishwa yana migogoro ya mipaka na kuna kesi mahakamani lakini pia hata bunge lilitaka kutatuliwa migogoro hiyo.

Wakili Alais Melau akizungumza na wanahabari hawapo pichani


“Novemba Waziri wa Ardhi, Angelina Mabula, akihutubia mkutano katika mji mdogo wa Ubaruku Wilaya ya Mbarali alitangaza kuwa vijiji na vitongoji 48 katika wilaya hiyo vilivamia Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kuviamuru viondoke mara moja. hata hivyo Serikali ilifanya kosa kuingiza ardhi ya vijiji na vitongoji hivyo kwenye hifadhi kwa tangazo namba 28 la mwaka 2008 bila kufuata sheria”alisema

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top