Na Elinipa Lupembe
Kituo cha afya cha Kivulini Martenity Afrika kimekuwa mkombozi wa wanawake wajawazito kwa kuwa kituo hicho ni kituo maalum cha kutoa huduma za kujifungua kwa kina mama wajawazito na matibabu ya wagonjwa wa fistula, kikifanikisha kupunguza vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua.
Kufuatia utoaji huduma hizo, Kivulini kimeongeza kujenga jengo la kupumzikia wajawazito wenye changamoto za uzazi na wale waliokaribia kujifungua kwa ajili ya kuwa na uangalizi wa karibu wa madaktari kwa mjazito, jengo lenye uwezo wa kupumzisha wajawazito 20, lililogharimu shilingi milioni 90.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo hilo, Mkurugenzi Mkazi Maternity Africa. Michael Hynds, amesema kuwa, lengo la kuongeza jengo hilo ni kupata wodi ua wapumzisha wajawazito waliokaribia kujifungua na wale wenye changamoto ili kuwa karibu na uangalizi wa madaktari.
"Tumefikia hatua hii, kutokana na changamoto iliyokuwa ya kukosa mahali pa kuwapumzisha wajawazito, jambo ambalo awali lilihatarisha maisha ya kina mama na watoto, lakini kuwepo kwa jengo hili, kutaokoa maisha ya mama na mtoto" . Amesisitiza Hinds.
Hata hivyo mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya Arusha, baada ya kuzindua jengo hilo, ameushukuru uongozi wa Kituo cha Maternity Afica kwa huduma bora za uzazi wanazozitoa kwa kina mama wa kitanzania, huduma ambazo zimesaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua katika halmashauri.
Mkurigenzi Msumi ameongeza kuwa, serikali inathamini huduma ya kipekee inayotolewa na kituo cha Kivulini, kituo ambacho kinafanya kazi kubwa yenye baraka za kiMungu zilizopaswa kufanywa na serikali na kuridhishwa namna wagonjwa wanapatiwa huduma bure bila malipo yoyote.
Muuguzi Mkuu, halmashauri ya Arudha Noemi Themi, amesema, kituo hicho kimepunguza msongamano wa wajawazito kwenye vituo vya serikali kwa mkoa wa Arusha na mikoa jirani, hususani wale wenye changamoto za uzazi na ugonjwa wa fistula.
Nao wagonjwa waliolazwa kwenye kituo hicho cha afya, wameponheza na kushukuru huduma bora inayotolewa hapo bila malipo yoyote ikiwemo, matibabu, malazi ma chakula, jambo ambalo limeokoa maisha ya familia zisizo na uwezo.
Suzana Msami (26) mkazi wa Muleba mkoani Kagera, amethibitisha kutibiwa ugonjwa wa Vistula, ugonjwa ambao alihangaika nao kwa muda mrefu kwenye hospitali za Muleba na Bugando bila mafanikio
"Nilipataa rufaa kutoka hospitali ya Bugando, na nimetibiwa kwa sasa ninaendelea vizuri, sikuwa na pesa za matibabu, hapa nimetibiwa bure na kupatiwa huduma za chakula na malazi bure, ninamshukuru Mungu ninawashukuru madaktari na wauguzi kwa upendo uliorejesha furaha na matumaini ya maisha yangu tena" .Amesisitiza Suzana
Kituo cha Afya Maternity Africa kilifunguliwa mwaka 2018 na mpaka sasa jumla ya akinamama 8500 wamejifunguliwa kituoni hapo huku zaidi ya wagonjwa 550 wametibiwa ugonjwa wa Fistula na wanategemea sasa kuhudumia zaidi ya wagonjwa elfu tatu kwa mwaka.
ARUSHA DC
KaziInaendelea
Post a Comment