Meneja
wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Kongwa Dodoma,Wilfredy Munisi
akizungumza wakati wa utamburisho wa wagei waliofika katika kituo hicho
kwa ajili ya hafla fupi ya utiaji saini katika makubaliano kati ya
TALIRI na Taasisi Binafsi ya kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya
kusaidia Wajasiliamali Vijana katika sekta ya Mifugo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed
Bohay (katikati) akizungumza wakati wa hafla fupi ya kutiliana saini
kati ya Taasisi hiyo na TALIRI ya kusaidia Wajasiliamali vijana.Kulia ni
Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na
kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt
Jonas Kizima.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed
Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt
Jonas Kizima wasaini Makubaliano kati ya Taasisi hizo
mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo .Kulia ni
Mkurugenzi wa Kituo cha Ubunifu katika Kilimo Biashara ,Tamim Amijee na
kushoto ni Meneja wa Kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa,Wilfredy Munisi.
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed
Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt
Jonas Kizima wasaini Makubaliano kati ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo .
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed
Bohay wakibadilishana faili na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa
Mifugo (TALIRI) Dkt Jonas Kizima zenye Makubaliano kati ya Taasisi hizo
mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya Mifugo .
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi Binafsi ya Kusaidia Sekta ya Kilimo nchini ,Nocomed
Bohay pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Dkt
Jonas Kizima wakionesha kwa wanahabari(hawako pichani) Makubaliano kati
ya Taasisi hizo mbili kusaidia Wajasiliamali vijana katika sekta ya
Mifugo .
Sehemu ya Mifugo (Mbuzi) inayofugwa katika kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa.
PASS imejipanga kusaidia katika uwekezaji wa miundombinu ya ufugaji wa Mbuzi yakiwemo Mabanda ya Kisasa.
Mbuzi wakitoka katika Mabanda yao.
Ng'ombe wakiwa katika kituo cha utafiti wa Mifugo -Kongwa.
Mmoja wa watumshi katika kituo cha Utafiti wa Mifugo Kongwa akimlambisha Ndama vidole vyake .
Sehemu ya Mabanda ya mbuzi yaliyopo katika kituo hicho.
Na Dixon Busagaga ,Dodoma.
TAASISI
ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI) imetumia fursa ya mkoa wa Dodoma kuwa
makao makuu ya nchi kuingia mashirikiano na Taasisi Binafsi ya kusaidia
Sekta ya Kilimo nchini ( PASS) ya kuwekeza katika sekta ya Mifugo kwa
kuwaandaa Wajasiliamali vijana.
Hatua
hiyo inatajwa kuondoa moja ya changamoto ya upatikanaji wa bidhaa ya
Nyama katika jiji la Dodoma ambalo kwa sasa idadi ya watu imeanza
kuongezeka baada ya ofisi na taasisi mbaimbali za serikali na umma
kuhamia Dodoma.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika
katika kituo cha Kongwa Dodoma ,Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Binafsi
ya kusaidia Sekta ya Kilimo Nchini(PASS) ,Nicomed Bohay alisema PASS
kupitia kituo cha ubnifu wa Biasharaza Kilimo wameamua kuanzisha Vituo
atamizi vya Mifugo katika kituo cha TALIRI Kongwa .
“Tumelenga
kuanza na mifugo aina ya Mbuzi katika kituo hiki ,zipo sababu
zilizotupelekea tuweze kuchagua eneo hili la Kongwa moja wapo ni uwep
wa soko la karibu ,… PASS tutawekeza kwenye Miundo mbinu ya ufugaji wa
Mbuzi ,pamoja na gharama za kuendesha mradi na malisho hadi mbuzi
watakapo weza kuuzwa sokoni .”alisema Bohay .
Alisema
kazi hiyo itafanyika kwa kutumia wajasiliamali Vijana wa Kitanzania
na kwamba utaratibu wa kuwapata vijana wenye sifa utatangazwa baadae na
watakao pata nafasi hiyo watapata nafasi ya kuunganishwa na taasisi za
kifedha kwa ajili ya kupata mitaji.
“Kwa
kuanza tumelenga kuanza na Unit 10 za mbuzi 100 ,kifupi tumepanga
kuanza na Mbuzi 1000 kwa mwaka huu ,nia yetu ni kwamba kutakuwa na
Wajasiliamali vijana kama 20,ambao kila mmoja atakuwa na Mbuzi kama
50,na tutaongeza mbuzi 1000 kila mwaka hadi kufikia Mbuzi 5000 ndani ya
kipindi cha miaka mitano ijayo.”alisema Bohay.
Bohay
alisema kwa kuanzia PASS imetenga kiasi cha sh Mil 500,katika
uwekezaji huo wa mwanzo kwa mifugo ya Mbuzi kutokana na uwepo wa
gharama kubwa katika ujenzi wa miundombinu yakiwemo Mabanda ya kisasa.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo,Dkt Jonas Kizima alisema ujio wa PASS
ni fursa muhimu kwa TALIRI kutumia utaalmau wa tafiti ili uweze kutumika
na Wajasiliamali katika sekta ya Mifugo nchini.
“Kituo
cha utafiti wa Mifugo ( TARIRI) kimesaini mkataba wa maelewano kwa
ajili ya kuandaa wajasiliamali katika sekta ya mifugo ,kwetu sisi ni
furaha inaipa nafasi sasa TALIRI ule ujuzi iliyonao ,zile Product
ilizonazo ziweze kwenda sasa kwa wadau wengine kibiashara .”alisema Dkt
Kizima.
Dkt
Kizima aliyataja maeneo hayo kuwa sasa Taasisi hiyo ya serikali ambayo
imejikita kwenye sekta ya mifugo itakuwa ni shamba darasa la
kuwaandaa wajasiliamali ambao sasa watapata fursa ya kujifunza masuala
mbalimbali yanayotolewa na TALIRI.
Alisema
jambo jingine TALIRI itatoa Mbegu kwa ajili ya Malisho ya Mifugo na
kwamba ujuzi utakaotolewa kwa wajasiliamali hao kwa kushirikiana na
Taasisi ya PASS utasaidia upatikanaji wa Wajasiliamali Wasomi katika
sekta ya Mifugo.
“Kitu
kingine taasisi ya utafiti wa mifugo (TALIRI) itapata nafasi ya
kuzitumia hizi takwimu za wajasiliamli kusambaza kwa wajasiliamli
wengine nchini ili wazitumie waone wanaweza kufuga kibiashara kukuza
uchumi wa nchi yetu,”alisema Dkt Kizima.
Taasisi
ya utafiti wa Mifugo (TALIRI)ina vituo saba vilivyotengwa kikanda
ambavyo ni TALIRI Kongwa-Dodoma ,TALIRI West Kilimanjaro,TALIRI Tanga
,TALIRI Naliendere Mtwara ,TALIRI Uyole-Mbeya,TARILI Mpwapwa na TALIRI
Mabuki ,Mwanza .
Post a Comment