- Wananchi watakiwa kuchangamkia fursa za wawekezaji Sekta ya Utalii
- Ni Baada ya Mwekezaji kutangaza kuwekeza sh 8.9 bilioni.
Wakazi
wa mkoa wa Simiyu na mikoa ya jirani, wametakiwa kuchangamkia fursa
zinazotokana na uwekezaji wa kampuni ya Kitalii ya Mwiba Holding Ltd
ambayo imewekeza katika pori la akiba la Meatu linalopakana na Mamlaka
ya hifadhi ya Ngorongoro.
Akizungumza
katika ziara ya kamati ya ulinzi na Usalama mkoa wa Simiyu na kamati ya
Siasa ya CCM mkoa wa Simiyu na wilaya ya Meatu katika eneo la
mwekezaji huyo, Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka alisema uwekezaji
wa kampuni hiyo umekuwa na faida kubwa kwa wananchi na taifa.
Alisema
kampuni hiyo, pia imekuwa ikichangia shughuli za maendeleo na hivi
karibuni, imetoa saruji mifugo 3000, mabati 1000 na zaidi ya sh 115
milioni kwa ajili ya kuchangia mfuko wa elimu wa mkoa.
"kama
kulikuwa na mahusiano mabaya baina ya vijiji na serikali na wawekezaji
hawa ambayo yalitokana na makosa ya watu wachache miaka ya nyuma sasa
tumeanza ukurasa mpya"alisema
Awali
Mmoja wa Wakurugenzi wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF)
ambayo kampuni zake ndizo zimewekeza katika wilaya hiyo ya Meatu,
Abdulkadir Mohamed, alisema hadi sasa kampuni zao, Mwiba Holding,
Tanzania Game Trackers Safaris(TGTS) na Wingert Safaris wamewekeza
zaidi ya bilioni 670 na mwaka huu wataongeza sh 227 bilioni.
"tunatarajia
kuongeza uwekezaji ila tunachoomba mazingira bora ya uwekezaji
kuondolewa migogoro katika maeneo yetu, ikiwepo uvamizi wa mifugo na
kama kuna mapungufu tuelezwe"alisema.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Simiyu,Enock Yakobo,alisema chama cha mapinduzi kwa sasa
hakina mgogoro na wawekezaji kwani mapungufu yaliyokuwepo yamekwisha na
mafanikio yanaonekana.
Hata
hivyo, Mwenyekiti huyo, alishauri Mwekezaji huyo, kusaidia ujenzi wa
mabweni kwa wanawafunzi wa kike katika shule ya Sekondari ya Makao.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa chama cha wafugaji taifa, Jackson Yuma
alitaka uongozi wa serikali kutokubali eneo la makao liharibiwe kwa
kuruhusu mifugo kwani ndani ya mwaka mmoja hali itakuwa mbaya.
Yuma
ambaye pia ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wa CCM mkoa wa Simiyu,
alitaka serikali kwa kushirikiana na wawekezaji kuhakikisha maeneo
yaliyotengwa katika uhifadhi yanatunzwa kwa gharama zote kwa faida ya
sasa na vizazi vijavyo.
Wakuu
wa wilaya za Meatu na Bariadi , wakizungumza katika ziara hiyo,
walishauri kuboreshwa mahusiano baina ya wananchi, wawekezaji na
serikali kwa manufaa ya mkoa wa Geita.
Mkuu wa wilaya ya Meatu Dk
Joseph Chilongani alisema wilaya yake na mkoa wa Simiyu tayari wameanza
kunufaika na wawekezaji wa sekta ya utalii na kutaka kuondolewa
migogoro isiyo ya lazima.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Bariadi, Festo Kuswaga alisema, taifa
linanufaika sana na sekta ya utalii ambayo ndiyo inaongoza kwa kuchangia
pato la taifa zaidi ya asilimia 18 na kuingiza fedha nyingi za kigeni
zaidi ya asilimia 25.
Post a Comment