Mwandishi wetu,Arusha.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi
waliovamia maeneo ya hifadhi nchini, kujiandaa kuondoka ndani ya miezi
mitatu kabla ya operesheni kuanza.
Akizungumza
na waandishi wa habari, katika eneo la hifadhi ya Jamii ya
wanyamapori(WMA) ya makao, wilayani Meatu, Dk Kigwangalla alisema
wavamizi wa maeneo ya hifadhi wengi wamekuwa wakijihusisha na matukio ya
ujangili.
"utakula
kijiji kina ardhi kubwa, lakini wengine wanajenga hadi katika ndani ya
eneo la mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na hao mara nyingi ndio
wanaingiza mifugo hifadhini usiku na kufanya ujangili"alisema
Alisema
maeneo mengi ya hifadhi na mapori ya akiba nchini yamevamia na wananchi
jambo ambalo serikali haiwezi kukubali yaharibiwe ama kutumika kwa
ujangili.
Waziri
huyo, pia alitembelea kambi ya kitalii ya TGTS na hoteli ya Mwiba na
kushuhudia vikosi vya kupambana na ujangili katika maeneo hayo ambavyo yapo chini ya taasisi Friedkin Conservation Fund na kueleza
kuridhishwa na uwekezaji wa taasisi hiyo.
Mkurugenzi
wa Mwiba Holding, Abdukaril Mohamed, alisema katika eneo la Mwiba
wamewekeza sh 2.2 bilion na hivi sasa wanaendelea na shughuli za
uhifadhi na utalii.
"mheshimiwa
Waziri katika eneo hili, kampuni yetu inafanya utalii wa picha na kuna
hoteli,tunafanyakazi kwa amani na utulivu na vijiji vinavyotuzunguka" alisema
Mwenyekiti
wa kijiji cha makao, Anthony Philip, alimweleza Waziri Dk Kigwangalla
kuwa, katika eneo hilo kuna mahusiano mazuri baina ya vijiji na
wawekezaji na vijiji vinapata mgao wa fedha.
Alisema
kijiji cha makao kimekuwa kikipata zaidi ya sh 147 milioni kwa mwaka
kutoka kwa mwekezaji na vijiji vingine sita vimekuwa vikipata zaidi ya
milioni 80,000 kila mwaka"alisema.
Akiwa
katika pori la akiba la Maswa,Meneja wa pori hilo, Lusato Masinde
alisema pia wanauhusiano mzuri na wawekezaji ambao licha ya kulipia ada
za vitalu pia wamekuwa wakitoa msaada wa huduma mbali mbali ikiwepo
maji.
Hata hivyo, alisema katika pori hilo changamoto kubwa ni uvamizi wa mifugo, uchache wa watumishi na upungufu wa vitendea kazi.
Post a Comment