WALINZI
wa wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa
yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wametakiwa kuwa makini na
waadilifu kutokana na kuongezeka kwa wanyama adimu wanaofika maeneo yao.
Rai
hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya
Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA) Meja Jenerali mstaafu Hamisi
Semfuko alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na ulinzi katika maeneo
hayo.
Meja
Jenerali Semfuko, alisema kazi ya kupambana na ujangili inahitaji
uvumilivu, uadilifu na ujasiri mkubwa kutokana na mazingira hatarishi
yaliyopo.
"La
muhimu kuna taatifa maeneo haya wameanza kuja wanyama adimu hivyo
ningependa muongeze jitihada hizi mara dufu wanyama hao wasidhurike,"
alisema.
Katika
ziara hiyo wajumbe wa Bodi ya TAWA walipokea taarifa ya timu ya pamoja
kati ya TAWA, Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), Frankfurt Zoological
Society ( FZS), TAWIRI na Friedkin Conservation Fund (FCF) katika
kuhifadhi na kulinda na kuhifadhi wanyama adimu.
Taarifa
hiyo iliyowasilishwa na wataalamu Philbert Ngoti wa TANAPA na Gerald
Nyaffi wa FZS katika eneo la kitalu kilichopo Maswa Mbono
kinachoendeshwa na kampuni ya Tanzania Game Tracker Safaris (TGTS).
Wataalam
hao walisema wamefanikiwa katika mradi huo kwa ufadhili wa familia ya
Friedkin inayomiliki TGTS ililiyofadhili fedha, vifaa pamoja na
helikopta, kazi ijayotarajiwa kuendelea katika maeneo mengine.
Katika
ziara hiyo TAWA imeridhishwa na utendaji wa Makampuni ya uwindaji na
upigaji picha za kitalii, yaliyopo katika maeneo yake kwa kusimamia
uhifadhi na ulinzi pamoja na kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi
yenye thamani zaidi ya sh 40 bilioni.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA),
Dk James Wakibara akizungumza na waandishi wa habari juu ya mchango kwa
jamii, uhifadhi na kiuchumi wa makampuni ya uwindaji wa kitalii
zilizowekeza katika maeneo yao.
Maeneo
yaliyotembelewa na TAWA ni pamoja na Hifadhi ya Jamii ya
Wanyamapori(WMA) ya Makao wilayani Meatu inayosimamiwa na kampuni ya
Mwiba Holdings Limited.
Dk
Wakibara alisema, licha mchango wa makampuni kwenye jamii, pia TAWA
kupitia malipo ya kampuni hizo, imekuwa ikitoa takriban sh 6.5 bilioni
kila mwaka kwa vijiji vyenye wawekezaji hao na halmashauri.
Makampuni
hayo yamewekeza katika baadhi ya maeneo ya vitalu 159 vilivyopo
nchini na maeneo ya hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA) 38 zilizopo
nchini.
"Hizi
kampuni za kitalii zina mchango mkubwa sana pia katika uhifadhi wa
maeneo haya, hasa katika vita dhidi ya ujangili ikizingatiwa asilimia 95
ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini yapo chini ya TAWA"alisema
Alisema
kwa sasa mapato ya TAWA kutokana na shughuli za uhifadhi, yamefikia
dola 20 lakini kuna mikakati ya kuongeza mapato hayo mara nne zaidi hadi
kufikia dola 80.
"kuna
dhana potofu kuwa uwindaji wa kitalii ni kumaliza wanyama hili sio
kweli, kwani haya makampuni hayajawahi kufikia hata robo kiwango cha
kuwinda wanyama ambacho kinatolewa kila mwaka na TAWA na mashirika ya
kimataifa"alisema
Mwenyekiti
wa bodi ya TAWA, Meja Jenerali mstaafu Hamisi Semfuko alisema mamlaka
hiyo ipo katika mabadiliko makubwa ili kuhakikisha jamii inanufaika
zaidi ya uhifadhi wa wanyamapori,katika kusaidia miradi ya kijamii ya
maji, afya Elimu na uhifadhi.
Mwenyekiti
huyo na bodi yake ambao walitembelea pori la Makao, lilipo mpakani mwa
Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Meatu,alisema wameridhishwa na
utendaji wa kampuni ya Mwiba Holding katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya
Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori nchini (TAWA), Meja Jenerali mstaafu
Hamisi Semfuko (wa pili kushoto mwenye miwani), akizungumza na walinzi wa
wanyamapori katika maeneo yanayozunguka Pori ya Akiba la Maswa mkoani Simiyu alipokua akikagua shughuli za uhifadhi na
ulinzi katika maeneo hayo.
Post a Comment