Ulinzi wa Faru katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti na maeneo ya
jirani, unatarajiwa kuimarika zaidi baada ya kuanza mradi maalum wa
Faru kufungwa vifaa vya technolojia za kisasa na hivyo kuwalinda na
matishio ya ujangili ama kupotea.
Faru
ni miongoni mwa wanyama ambao wapo hatarini, kutoweka duniani, kutokana
na kuwindwa na majangili, ambao wamekuwa wakiuza pembe zao na hivyo
serikali imekuwa na mikakati kadhaa ya kuimarisha ulinzi wao.
Akizungumza
na wanahabari, Mwakilishi mkazi wa shirika la uhifadhi la kimataifa
la Frankfurt zoological Society moja ya mashirika yanayoratibu mradi
huo, Gerald Bigulube alisema mradi huo wa aina yake barani Afrika,
unatarajiwa kuimalisha ulinzi na ufatiliaji wa faru katika eneo la
Seregeti.
Alisema mradi
huo unatarajiwa kutumia zaidi ya sh 253 milioni, zilizotolewa na shirika
la uhifadhi la Friedkin Conservation Fund(FCF) na unaratibiwa pia na
Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) na Taasisi ya utafiti wa
Wanyamapori(TAWIRI).
Bigulube
alisema, tayari utekelezaji wa mradi huo, umeanza, ambapo mwaka jana
faru 21 walifungwa vifaa maalum digital VHF na mwaka huu wengine
watafungwa vifaa vya kisasa zaidi kutumia mfumo wa LoRa(LoRa System).
"lengo
letu kama wahifadhi ni kuhakikisha Faru waliopo nchini wanaongezeka
zaidi sambamba na wanyama wengine ambao maisha yao yamekuwa hatarini
wakiwepo Tembo ambao nao tayari kuna miradi ya kuwafunga vifaa vya
kisasa ili kuwafatilia
"alisema
Alisema
katika kuhakikisha mradi huo unakuwa endelevu wameanza kuwapeleka
kwenye mafunzo wahifadhi nchini Uholanzi ambao ndio watakuwa wakiratibu
matumizi ya technolojia katika ulinzi na ufatiliaji wa faru.
"hivi
karibuni tutaanza kuwafunga vifaa Faru, zoezi ambalo litatumia
techolojia za hali ya juu,helkopta nna vifaa vingine vya kisasa kama
ilivyokuwa mwaka jana"alisema.
Akizungumzia
mradi huo, Mhifadhi Mkuu wa hifadhi za Taifa ya Serengeti, William
Mwakilema alisema, mpango huo ambao unashirikisha wizara ya maliasili na
utalii na wadau wengine utasaidia sana ulinzi wa Faru.
"Ulinzi
wa Faru ni jambo ambalo ni nyeti na serikali na vyombo vyake imekuwa
ikifatilia kwa makini hivyo,lengo kuu ni kuhakikisha
wanahifadhiwa"alisema
Mtafiti
kiongozi wa taasisi ya utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI),Dk Edward Kohi
,alisema ili kuimarishwa ulinzi wa faru, technolojia mbali mbali
zinatakiwa kutumika.
"hii
ni technolojia ya kuwafunga vifaa maalum, itawezesha kujulikana kila
siku wapo wapi na hivyo ni rahisi kuwafatilia na kuwapa ulinzi"alisema
Tanzania
ni miongoni mwa mataifa machache duniani, ambayo bado yana idadi kubwa
wa faru ambao wamehifadhiwa katika hifadhi kadhaa za taifa, tofauti za
nchini nyingine ambazo zimehifadhi Faru katika mashamba maalum ya
wanyama.
Post a Comment