PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WAZIRI WA MAMBO YA NJE UJERUMANI ATAEMBELEA TAASISI ZA UN TANZANIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas  (katikati) akiwa katika Mahakama za jinai za umoja wa mataifa  zilizoko eneo la Laki lak...
Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas  (katikati) akiwa katika Mahakama za jinai za umoja wa mataifa  zilizoko eneo la Laki laki jijini Arusha Tanzania ,kushoto ni Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama  hiyo Sera Attika .Kulia ni Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo  Ousman Njikam

Msajili wa Mahakama ya jinai ya Umoja wa Mataifa UN nchini Tanzania  Sera Attika akifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas  ,katikati ni Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo  Ousman Njikam ,kufuatia ziara ya kwanza ya Wwaziri huyo kutembelea Taasisi ya  Umoja wa Mataifa  (UN) ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa  zilizoko eneo la Laki laki .Picha na Ferdinand Shayo

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas  akisaini kitabu cha wageni ali[powasili katika katika Taasisi ya  Umoja wa Mataifa  (UN) ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa  zilizoko eneo la Laki laki jijini Arusha nchini  Tanzania .Kulia kwake ni  Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama Sera Attika . Picha na Ferdinand Shayo


 Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas  akiwasili katika katika Taasisi ya  Umoja wa Mataifa  (UN) ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa  zilizoko eneo la Laki laki jijini Arusha Tanzania,wapili  kulia ni  Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo  Ousman Njikam ,kushoto ni  Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama Sera Attika .Picha na Ferdinand Shayo


Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas ametembelea Ofisi za Umoja wa Mataifa ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa pamoja na kujionea makavati yaliyowekwa kumbukumbu za upelelezi,mashtaka na mwenendo wa kesi.
Waziri huyo aliambatana na  balozi za Ujerumani nchini Tanzania alipokuwa katika ziara yake ya siku moja ambapo alipata kujulishwa juu ya shughuli za za taasisi hiyo ambayo imejikita katika kuwasaka watuhumiwa ambao bado hawajakamatwa ,kuwalinda waathirika na mashahidi wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.
Ziara ya waziri huyo ni ziara ya kwanza barani Afrika  tangu ateuliwe kuwa waziri march 2018 ,ziara hiyo ni muendelezo wa Nchi ya Ujerumani ambapo amesema kuwa wanafurahi  katoa mchango kwa taasisi hiyo ya kimataifa pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya  Ujerumani na bara la Afrika.
Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo  Ousman Njikam amemkaribisha Waziri huyo katika jengo la mahakama ambapo shughuli za kimahakama zinaendeshwa ,mahakama hiyo inaendelea na kazi yake ili kutoa haki kwa walalamikaji na walalamikiwa .
Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama Sera Attika amesema kuwa mahakama hiyo ina sehemu maalumu za maabusu,na maktaba yenye makavati yaliyobeba historia ya Mauaji ya Rwanda ambayo hutumika kwa utafiti .
Waziri huyo ametembelea taasisi za kimaitaifa ikiwemo Mahakama ya Haki za binadamu ya Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top