Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Miss
Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni
mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini Afrika ya
Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma mwishoni mwa wiki kwa
ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss
Journalism yatakayofanyika Jijini Arusha mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha,
amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa utalii wa Pori la Akiba
Selous.
Na Hamza Temba-WMU-Dodoma
.............................. .............................. .................
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amemteua mshindi wa taji
la Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) kuwa
balozi wa utalii wa Pori la Akiba Selous.
Amefanya
uteuzi huo mwishoni mwa wiki Jijini Dodoma baada ya mazungumzo na
mwanamitindo huyo aliyemtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kuomba
ufadhili wa kuandaa mradi wa kijamii ambao ni sehemu ya shindano
atakaloshiriki la taji la Dunia la Miss Journalism 2018 litakalofanyika
Oktoba 27 Jijini Arusha.
Kufuatia
uteuzi huo, Dk. Kigwangalla amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya
Utalii Tanzania, Devotha Mdachi kuandika barua ya uteuzi kwa balozi huyo
mpya sambamba na kumkabidhi hati ya uteuzi ili pamoja na mambo mengine
aweze kunadi vivutio vya utalii vya pori hilo.
Wakati
huo huo, Dk. Kigwangalla amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, Dk. James Wakibara kuandaa
safari maalum ya balozi huyo mteule aweze kutembelea Pori la Akiba
Selous kwa ajili ya kuona na kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu
hifadhi hiyo kwa ajili ya utangazaji.
Sambamba
na pori hilo atatembelea pia mapori mengine ikiwemo BBK (Burigi,
Biharamulo na Kimisi) mkoani Kagera na Mpanga Kipengele mkoani Njombe
ambapo atatumia fursa hiyo kufanya mahojiano na wasichana wa vijiji
jirani na hifadhi hizo kwa ajili ya mradi wa kijamii wa kuwainua ikiwa
ni sehemu yenye alama muhimu kwenye shindano hilo la Dunia la Miss
Journalism 2018.
Awali
akiwasilisha ombi lake kwa Waziri Kigwangalla la ufadhili wa safari
yake ya ushiriki wa mashindano hayo, Witness pia aliomba kupewa fursa ya
kuwa balozi wa Tanzania kwenye moja ya sekta ikiwemo Misitu, Nyuki au
Utalii.
Mbali
na kushikilia taji la Miss Journalism Tanzania 2018, Witness amesema
amewahi kushinda mataji mengine manne makubwa ya kimataifa ya ulimbwende
nchini Afrika ya Kusini anakosomea urubani kwa sasa.
Anasema,
"Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Garden Route 2017, ambalo ni taji la
kitaifa la kuhamasisha na kukuza sekta ya Maliasili na Utalii nchini
humo, licha ya kuwa ugenini nilitumia fursa hiyo kunadi vivutio vya
utalii vya Tanzania.
"Mashindano
haya yalihusisha washiriki 600 na wote walikuwa na asili ya kizungu,
mimi peke yangu nilikuwa na asili ya kiafrika na niliibuka mshindi".
Aliyataja
mataji mengine kuwa ni Miss Bees Cape Town 2017 kwa ajili kuhamasisha
uhifadhi wa sekta ya nyuki na mataji mawili ya kimkoa ambayo ni Miss
Asla Capetown 2017 na Miss Carnival Mosselbay 2017.
Mataji
mengine ya kitaifa aliyowahi kushinda Witness hapa nchini ni pamoja na
Miss Arusha Higher Learning 2014 na Miss Northern Zone 2014.
Mashindano
hayo ya Dunia ya Miss Journalism 2018 yanahusisha pia uhamasishaji wa
maendeleo ya utalii, utamaduni wa amani, uandishi wa habari na kupiga
vita ugonjwa wa ukimwi na Malaria.
Pori
la akiba Selous ndio hifadhi kubwa kuliko zote nchini ikiwa na ukubwa
wa kilomita za mraba takriban 50,000 katika mikoa ya Pwani, Morogoro,
Lindi, Mtwara na Ruvuma. Mwaka 1982, Shirika la Umoja wa Mataifa la
Elimu, Sayansi na Utamaduni (Uneso) lilitangaza eneo hilo kuwa moja ya
eneo la Urithi wa Dunia na kuanza kuhifadhiwa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akionyeshwa taji la
urembo la "Miss Garden Route South Africa 2017" ambalo ni maalum kwa
ajili ya kuhamasisha utalii nchini Afrika ya Kusini na Miss Journalism
Tanzania 2018, Witness Teddy Kavumo (21) aliyeshinda taji hilo na mataji
mengine matatu nchini humo mwaka jana, alipomtembelea ofisini kwake
mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki kwenye
mashindano ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jijini Arusha
mwezi Oktoba mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa
vivutio vya utalii vya Pori la Akiba Selous.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa kwenye picha ya
pamoja na Miss Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21)
ambaye pia ni mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo
nchini Afrika ya Kusini, alipomtembelea ofisini kwake Jijini Dodoma
mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano
ya Dunia Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba
mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa vivutio vya
utalii vya Pori la Akiba Selous.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Miss
Journalism Tanzania, 2018, Witness Teddy Kavumo (21) ambaye pia ni
mshindi wa mwaka jana wa mataji manne ya Uanamitindo nchini Afrika ya
Kusini, baada ya mazungumzo ofisini kwake Jijini Dodoma alipomtembelea
mwishoni mwa wiki kwa ajili ya kuomba ufadhili wa kushiriki mashindano
ya Dunia ya Miss Journalism yatakayofanyika Jinini Arusha mwezi Oktoba
mwaka huu. Aidha, amemteua mwanamitindo huyo kuwa balozi wa wa utalii wa
Pori la Akiba Selous.
Post a Comment