PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: WATUHUMIWA WA UTEKAJI WA MWANDISHI WA HABARI ARUSHA KUSOTA MAGEREZA KWA UNYANG'ANYI WA KUTUMIA SILAHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Ofisa Itifaki wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Swalehe Mwidadi na mfanyakazi wa Masijala Amina Mshana leo May ...



Ofisa Itifaki wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Swalehe Mwidadi na mfanyakazi wa Masijala Amina Mshana leo May 23, 2018 wamepanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha na kusomewa shtaka la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa serikali Sabina Silayo mbele ya Hakimu Mkazi Patricia Kisinda, amedai kuwa watuhumiwa hao kwa pamoja wanashtakiwa kwa makosa mawili.

Amedai kuwa kosa la kwanza, wametenda mnamo May 13, 2018 eneo la Sakina washtakiwa hao walimwibia Mwandishi wa Habari wa kujitegemea Lucas Myovela simu aina ya Tekno  C7 ya thamani ya Sh.300,000,  simu aina ya Sumsung yenye thamani ya Sh.50,000 na walifanya unyang”anyi huo kwa kutumia panga na mkanda wa plastiki.

Aliendelea kutaja kuwa vitu vingine walivyoiba ni pamoja na fedha taslimu Sh.75,000 na walijihamishia fedha Sh.9,500 za Mpesa na kadi ya ATM ya benki ya CRDB, huku wakijuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Silayo alidai kuwa kosa la pili  wanashtakiwa kuwa mnamo May 13, 2018, eneo la Sakina kwa pamoja walifanya kitendo cha ukatili na udhalilishaji kwa kumvua Lucas Myovela nguo zake na kumchukua picha akiwa uchi.
Alidai kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na kufunguliwa kesi hiyo namba 153/2018.

Washtakiwa walikana mashtaka hayo na Wakili Silayo amedai upelelezi haujakamilika na kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.
Hakimu Kisinda amedai kesi hiyo haina dhamana na shtaka la kwanza halina dhamana hivyo alipanga kutajwa tena June 5 mwaka huu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top