Akichangia mjadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ya mwaka 2018/19, Bulaya amesema fedha zinazotengwa hazitolewi.
Amesema hayo jana Mei 7, 2018 kuwa, kuna hospitali zinashindwa kufanya upasuaji kwa kukosa maji, huku wanawake wakipata adha.
Mbunge huyo amesema wabunge na mawaziri wakikatiwa maji watahisi uchungu wanaopata wananchi wa kukosa maji safi na salama.
Amesema ilivyo sasa ni bora mgonjwa akapelekewa ndoo ya maji kuliko chakula.
Bulaya amesema hata vijana wanapohamasishwa kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji kama hakuna maji ni kazi bure.
“Tunaguswa na tatizo la Watanzania, tunaguswa na tatizo la ajira kwa vijana, ambao wanakwenda kuwekeza katika kilimo lakini hakuna maji,” amesema.
Post a Comment