Mhifadhi
Mkuu wa hifadhi ya taifa ya Tarangire,Herman Batiho akizungumza na wanahabari juu ya kukabiliwa na changamoto ya kubaki kisiwa kutokana na uvamizi wa watu katika baadhi ya maeneo ya hifadhi hiyo |
Mhifadhi
Mkuu wa hifadhi ya taifa ya Tarangire,Herman Batiho akizungumza na wanahabari juu ya kukabiliwa na changamoto ya kubaki kisiwa kutokana na uvamizi wa watu katika baadhi ya maeneo ya hifadhi hiyo |
Afisa mifugo na uvuvi halmashauri ya Babati vijijini Bwana Gilbert Mbesere akizungumza na wanahabari hao |
Mkurugeni wa chemchem foundation Ricardo Toss akizungumza na wanahabari hao juu ya changamoto zinazotokana na shughuli za jamii katika maeneo hayo |
Charles sylvester meneja wa chemchem foundation akizungumza na wanahabari hao |
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT
Taasisi
ya Utafiti wa Wanyamapori(TAWIRI),imeombwa kusaidia kuanisha maeneo ya
mapito ya wanyama katika eneo la Ikolojia ya Tarangire na Manyara, ili
kuzuia uharibifu na uvamizi wa maeneo hayo ambao unaendelea.
Eneo
la ikolojia ya Tarangire na Manyara lina ukubwa kwa kilomita za mraba
35,000 ambapo sasa eneo kubwa la nje ya hifadhi limevamiwa na shughuli
za kibinaadamu,ikiwepo kilimo, ufugaji na makazi.
Afisa
Wanyamapori wa halmashauri ya Babati vijijini, Beatrice Ndanu,
akizungumza na waandishi wa habari, alisema baada ya wizara ya Maliasili
na Utalii, kutoa kanuni za ulinzi wa mapito ya wanyamapori, sasa
wanasubiri TAWIRI kuanisha mapito hayo ili yasimamiwe.
Ndanu
alisema, katika eneo la ikolojia ya Tarangire na Manyara, kuna uvamizi
mkubwa wa shughuli za kibinaadamu,ikiwepo wafugaji,kuanzisha mashamba,
majengo na kilimo.
Mkurugenzi
wa taasisi ya uhifadhi ya Chemchem foundation, Riccardo Tossi, ambao
wamewekeza katika eneo la hifadhi ya jamii ya Burunge lilipo kati kati
yaTarangire na Manyara, alisema wapo tayari kushirikiana na serikali
kuwezesha kuanishwa maeneo ya mapito ya nyama.
"tunapata
shida katika uwekezaji, kuna mifugo na makazi ndani ya hifadhi hivyo
imekuwa ni changamoto katika kupambana na ujangili"alisema
Mhifadhi
Mkuu wa hifadhi ya taifa ya Tarangire,Herman Batiho alisema hifadhi
hiyo ambayo iliyoanzishwa mwaka 1970, ikiwa na ukubwa wa kilomita za
mraba 2850 inakabiliwa na changamoto ya kubaki kisiwa kutokana na
uvamizi wa watu.
Alisema
watu wamevamia maeneo ya mapito ya wanyama na kufanya shughuli za
kibinadamu ambazo zina athari kwa wanyamapori na kuendelea kuwepo hifadi
hizo.
"tunaomba
mapito ya wanyama kuanishwa na kulindwa lakini pia kudhibiwa watu ambao
wamekuwa wakiharibu vyanzo vya maji na kufanya shughuli ikiwepo kilimo
na ufugaji katika maeneo ya hifadhi"alisema
Mwenyekiti
wa jumuiya ya hifadhi ya jamii ya wanyamapori(WMA) ya BURUNGE, Ismail
Ramadhani, alisema ongezeko la watu na mifugo,imekuwa ni tatizo katika
uhifadhi hasa kutokana na kuongezeka uvamizi katika maeneo
yaliyohifadhiwa.
Hata
hivyo, alisema hivi sasa kuna mkakati wa vijiji vyote ambavyo vipo
katika eneo la Burunge WMA, kupimwa na kuanzisha mpango wa matumizi
bora ya ardhi, ambayo itawezesha kutengwa maeneo ya hifadhi na shughuli
za kijamii.
Post a Comment